Kukojoa kitandani ni tatizo la kawaida miongoni mwa watoto wadogo wakati mwingine wapo hata watu wazima wanaokabiliwa na tatizo hili.
Ni kitendo cha kutokujitakia cha kutoa mkojo ukiwa usingizini kitandani. Ingawa ni jambo linalohuzunisha sana hata hivyo ni jambo la kawaida kwa watoto wadogo mpaka miaka 6.
Watoto huwa hawafanyi kitendo hiki kwa kujipendea au sababu ni wavivu, hapana, ni matatizo yaliyopo kwenye kibofu cha mkojo ikiwemo:
Kuwa na kibofu kidogo cha mkojoKuchelewa kukua au kukomaa kwa kibofu cha mkojoUzalishwaji uliozidi wa mkojo,U.T.I ( yutiai)Mfadhaiko (stress)Kufunga choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu kwa kipindi kirefuUsawa usiosawa wa homoni.
Watoto kwa kawaida hupata usingizi mzito sana kila siku sababu ya michezo yao ya kutwa nzima na hivyo ubongo wao haupati ishara za kutosha za kibofu cha mkojo kujaa. Pia katika baadhi ya watoto tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa ni jambo la kurithi toka kwa wazazi wao.
Kadri mtoto anavyokuwa mkubwa ndivyo na tatizo la kukojoa kitandani linavyopungua. Wakati mwingine hili linaweza kuendelea hata ukubwani na hivyo kuwa shida kwa mtoto mwenyewe, wazazi wake na jamii inayomzunguka kwa ujumla.
Unaweza kumsaidia mwanao aache kukojoa kitandani kwa kutumia baadhi ya dawa hizi asili 8 hapa chini, chagua inayopatikana kirahisi mahali ulipo na uitumie, hata hivyo dawa namba 1 ni mhimu itumike sambamba na nyingine moja au mbili kwa matokeo mazuri zaidi.
Dawa za asili 8 zinazotibu tatizo la kukojoa kitandani
1. Maji ya Kunywa
Ikiwa mtoto au hata mtu mzima mwenye tatizo hili atakunywa maji kabla ya kwenda kulala (ndiyo namaanisha kabla ya kwenda kulala usidhani nimekosea) basi hataweza kukojoa kitandani tena akiwa usingizini.
Kile unatakiwa kufanya ni kunywa maji mengi zaidi kila siku kutwa nzima kidogo kidogo.
Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha hydrogen na nitrogen kwa pamoja na kuunda amonia. Amonia ni sumu katika mwili wa binadamu. Wakati ubongo unapopata ujumbe kutoka kwenye kibofu cha mkojo, ubongo humfanya mtoto aote kwamba yupo chooni na hatimaye hukojoa akiwa usingizini.
Huku yupo usingizi bado ataona wazi yupo chooni sababu ya hiyo ammonia.
Kwahiyo sababu ya mtu kukojoa kitandani ni matokeo ya kuundwa kwa amonia kwenye kibofu cha mkojo na amonia hii inaondolewa kirahisi mwilini kwa kunywa maji mengi kila siku.
Watu wengi hawanywi maji ya kutosha kila siku, wengi kama siyo wote wanasubiri KIU ndipo wanywe maji jambo ambalo ni kosa. Kiu ni ISHARA ya mwili iliyoCHELEWA ya kuhitaji maji.
2. Mdalasini
Mdalasini ni dawa rahisi zaidi kwa mtoto anayekojoa kitandani. Inaaminika kwamba kiungo hiki huufanya mwili kuwa wa moto moto.
Chukua mdalasini ya unga kama kijiko kidogo kimoja hivi cha chai changanya na asali kijiko kidogo tena na upake kwenye kipande cha mkate na umpe mtoto ale kila siku wakati wa chai ya asubuhi
3. ZabibuBata (Indian Gooseberry)
ZabibuBata ambazo pia hujulikana kama amla ni dawa nyingine ya kihindi nzuri kwa ajili ya tatizo hili la kukojoa kitandani.
Chukua zabibubata 2 kisha ondoa ganda lake la nje na uziponde kidogo, halafu changanya pamoja na kijiko kidogo cha chai cha asali na kiasi kidogo cha binzari ya unga. Mpe mtoto kijiko kidogo cha chai cha mchanganyiko huu kila siku asubuhi mpaka atakapopona.
4. Masaji
Masaji pia inatibu tatizo la kukojoa kitandani na kwa matokeo mazuri zaidi tumia mafuta ya zeituni (olive oil).
Yapashe moto kidogo mafuta ya zeituni ili yawe ya uvuguvugu kwa mbali na upake ya kutosha sehemu ya chini ya tumbo la mtoto na ufanye masaji eneo hilo polepole kwa dakika kadhaa.
Fanya zoezi hili kila siku mpaka umeridhika na mtokeo yake.
5. Jozi (Walnuts) na ZabibuKavu (Raisins)
Jozi na Zabibu kavu vinaweza pia kutumika kupunguza tatizo la kukojoa kitandani. Watoto wengi watafurahia pia kutumia kwani hivi ni vitu vya asusa (snack).
Mpe mtoto jozi 2 na zabibu kavu 5 kabla ya kwenda kulala kila siku kwa wiki kadhaa mpaka umeanza kuona mabadiliko.
6. Asali mbichi
Dawa nyingine maarufu kutibu tatizo la kukojoa kitandani ni asali mbichi. Watoto wengi wanapenda radha tamu ya asali na hivyo ni rahisi kutumika kwao kama dawa.
Mpe mtoto kijiko kidogo kimoja cha chai cha asali mbichi kila anapoenda kulala kila siku mpaka atakapopona. Unaweza pia kuchanganya na maziwa fresh wakati wa chai ya asubuhi.
7. Siki ya tufaa (Apple Cider Vinegar)
Siki ya tufaa husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la kukojoa kitandani.
Siki ya tufaa pia husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.
Mimina vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya kunywa na umpe mtoto anywe kutwa mara 1 kila siku, unaweza pia kuongeza asali kidogo ndani yake kupata radha. Vizuri akinywa wakati wakula chakula cha mchana au cha jioni.
8. Mbegu za Mharadali (Mustard Seeds)
Dawa nyingine nzuri kwa tatizo la kukojoa kitandani ni mbegu za mharadali. Ni dawa nzuri pia kwa wale wenye tatizo la U.T.I (yutiai).
Weka nusu kijiko kidogo cha chai cha mbegu za mharadali au unga wa mbegu hizi ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa fresh asubuhi na umpe mtoto anywe kinywaji hiki lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kila siku mpaka amepona.
Mambo ya mhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hizi:
• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mtoto muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.
• Mhimize mtoto kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku
• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtoto akiona giza anaogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini.
• Mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani, hii itamuongezea nguvu na moyo zaidi wa kujidhibiti zaidi na tatizo lake.
• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni.
• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi, malta, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti
• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.
• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.
Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tama haraka.
No comments:
Post a Comment