Showing posts with label Ushauri. Show all posts
Showing posts with label Ushauri. Show all posts

Tuesday, April 4, 2017

Suluhisho la kukojoa kitandani

Kukojoa kitandani ni tatizo la kawaida miongoni mwa watoto wadogo wakati mwingine wapo hata watu wazima wanaokabiliwa na tatizo hili.

Ni kitendo cha kutokujitakia cha kutoa mkojo ukiwa usingizini kitandani. Ingawa ni jambo linalohuzunisha sana hata hivyo ni jambo la kawaida kwa watoto wadogo mpaka miaka 6.

Watoto huwa hawafanyi kitendo hiki kwa kujipendea au sababu ni wavivu, hapana, ni matatizo yaliyopo kwenye kibofu cha mkojo ikiwemo:

Kuwa na kibofu kidogo cha mkojoKuchelewa kukua au kukomaa kwa kibofu cha mkojoUzalishwaji uliozidi wa mkojo,U.T.I ( yutiai)Mfadhaiko (stress)Kufunga choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu kwa kipindi kirefuUsawa usiosawa wa homoni.

Watoto kwa kawaida hupata usingizi mzito sana kila siku sababu ya michezo yao ya kutwa nzima na hivyo ubongo wao haupati ishara za kutosha za kibofu cha mkojo kujaa. Pia katika baadhi ya watoto tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa ni jambo la kurithi toka kwa wazazi wao.

Kadri mtoto anavyokuwa mkubwa ndivyo na tatizo la kukojoa kitandani linavyopungua. Wakati mwingine hili linaweza kuendelea hata ukubwani na hivyo kuwa shida kwa mtoto mwenyewe, wazazi wake na jamii inayomzunguka kwa ujumla.

Unaweza kumsaidia mwanao aache kukojoa kitandani kwa kutumia baadhi ya dawa hizi asili 8 hapa chini, chagua inayopatikana kirahisi mahali ulipo na uitumie, hata hivyo dawa namba 1 ni mhimu itumike sambamba na nyingine moja au mbili kwa matokeo mazuri zaidi.

Dawa za asili 8 zinazotibu tatizo la kukojoa kitandani

1. Maji ya Kunywa
Ikiwa mtoto au hata mtu mzima mwenye tatizo hili atakunywa maji kabla ya kwenda kulala (ndiyo namaanisha kabla ya kwenda kulala usidhani nimekosea) basi hataweza kukojoa kitandani tena akiwa usingizini.

Kile unatakiwa kufanya ni kunywa maji mengi zaidi kila siku kutwa nzima kidogo kidogo.

Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha hydrogen na nitrogen kwa pamoja na kuunda amonia. Amonia ni sumu katika mwili wa binadamu. Wakati ubongo unapopata ujumbe kutoka kwenye kibofu cha mkojo, ubongo humfanya mtoto aote kwamba yupo chooni na hatimaye hukojoa akiwa usingizini.

Huku yupo usingizi bado ataona wazi yupo chooni sababu ya hiyo ammonia.
Kwahiyo sababu ya mtu kukojoa kitandani ni matokeo ya kuundwa kwa amonia kwenye kibofu cha mkojo na amonia hii inaondolewa kirahisi mwilini kwa kunywa maji mengi kila siku.

Watu wengi hawanywi maji ya kutosha kila siku, wengi kama siyo wote wanasubiri KIU ndipo wanywe maji jambo ambalo ni kosa. Kiu ni ISHARA ya mwili iliyoCHELEWA ya kuhitaji maji.

2. Mdalasini
Mdalasini ni dawa rahisi zaidi kwa mtoto anayekojoa kitandani. Inaaminika kwamba kiungo hiki huufanya mwili kuwa wa moto moto.

Chukua mdalasini ya unga kama kijiko kidogo kimoja hivi cha chai changanya na asali kijiko kidogo tena na upake kwenye kipande cha mkate na umpe mtoto ale kila siku wakati wa chai ya asubuhi

3. ZabibuBata (Indian Gooseberry)
ZabibuBata ambazo pia hujulikana kama amla ni dawa nyingine ya kihindi nzuri kwa ajili ya tatizo hili la kukojoa kitandani.

Chukua zabibubata 2 kisha ondoa ganda lake la nje na uziponde kidogo, halafu changanya pamoja na kijiko kidogo cha chai cha asali na kiasi kidogo cha binzari ya unga. Mpe mtoto kijiko kidogo cha chai cha mchanganyiko huu kila siku asubuhi mpaka atakapopona.

4. Masaji
Masaji pia inatibu tatizo la kukojoa kitandani na kwa matokeo mazuri zaidi tumia mafuta ya zeituni (olive oil).

Yapashe moto kidogo mafuta ya zeituni ili yawe ya uvuguvugu kwa mbali na upake ya kutosha sehemu ya chini ya tumbo la mtoto na ufanye masaji eneo hilo polepole kwa dakika kadhaa.

Fanya zoezi hili kila siku mpaka umeridhika na mtokeo yake.

5. Jozi (Walnuts) na ZabibuKavu (Raisins)
Jozi na Zabibu kavu vinaweza pia kutumika kupunguza tatizo la kukojoa kitandani. Watoto wengi watafurahia pia kutumia kwani hivi ni vitu vya asusa (snack).

Mpe mtoto jozi 2 na zabibu kavu 5 kabla ya kwenda kulala kila siku kwa wiki kadhaa mpaka umeanza kuona mabadiliko.

6. Asali mbichi
Dawa nyingine maarufu kutibu tatizo la kukojoa kitandani ni asali mbichi. Watoto wengi wanapenda radha tamu ya asali na hivyo ni rahisi kutumika kwao kama dawa.

Mpe mtoto kijiko kidogo kimoja cha chai cha asali mbichi kila anapoenda kulala kila siku mpaka atakapopona. Unaweza pia kuchanganya na maziwa fresh wakati wa chai ya asubuhi.

7. Siki ya tufaa (Apple Cider Vinegar)
Siki ya tufaa husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la kukojoa kitandani.

Siki ya tufaa pia husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.

Mimina vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya kunywa na umpe mtoto anywe kutwa mara 1 kila siku, unaweza pia kuongeza asali kidogo ndani yake kupata radha. Vizuri akinywa wakati wakula chakula cha mchana au cha jioni.

8. Mbegu za Mharadali (Mustard Seeds)
Dawa nyingine nzuri kwa tatizo la kukojoa kitandani ni mbegu za mharadali. Ni dawa nzuri pia kwa wale wenye tatizo la U.T.I (yutiai).

Weka nusu kijiko kidogo cha chai cha mbegu za mharadali au unga wa mbegu hizi ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa fresh asubuhi na umpe mtoto anywe kinywaji hiki lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kila siku mpaka amepona.

Mambo ya mhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hizi:
• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mtoto muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.

• Mhimize mtoto kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku

• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtoto akiona giza anaogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini.

• Mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani, hii itamuongezea nguvu na moyo zaidi wa kujidhibiti zaidi na tatizo lake.

• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni.

• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi, malta, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti

• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.

• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.

Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tama haraka.  

Thursday, March 30, 2017

ONDOA SUMU MWILINI KWA NJIA zifuatazo

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng'enyo wa chakula mwilini mwako.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

-Uchovu sugu
-Maumivu ya maungio
-Msongamano puani
-Kuumwa kichwa kila mara
-Tumbo kujaa gesi
-Kufunga choo au kupata choo kigumu
-Kukosa utulivu
-Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
-Pumzi mbaya
-Mzunguko wa hedhi usio sawa
-Kuishiwa nguvu
-Kushindwa kupungua uzito
-Kupenda kula kula kila mara

Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini

1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee

Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi. Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee.

2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani

Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani  au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Fanya masaji

Kwa bahati mbaya waTanzania wengi hawajuwi kuwa masaji ni sehemu ya tiba au ni dawa pia kwa magonjwa mengine mengi mwilini. Wengi tunaichukulia masaji kama kitu cha starehe tu (relaxation) lakini unaweza kutumia masaji kama njia mojawapo ya kuondoa sumu mwilini na utafanikiwa kwa muda mfupi sana.

4. Kunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni. Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo. Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo ili kusafisha damu na mwili kwa ujumla ni lazima unywe maji ya kutosha kila siku.

5. Acha chai ya rangi na Kahawa

Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa. Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai. Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake. Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

6. Fanya mazoezi ya viungo

Inashangaza sana kuona waTanzania wengi hawaoni umhimu wa kufanya mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo ni jambo la lazima kama ilivyo chakula. Iwe unaumwa au huumwi, iwe una uzito kuzidi au una uzito wa kawaida hakikisha unapata muda wa kufanya mazoezi.

Mazoezi yanakusaidia kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kukuondolea mfadhaiko au stress kirahisi zaidi, sambamba na hilo mazoezi ni dawa tosha na nzuri ya kuondoa sumu mwilini haraka zaidi. Hakikisha jasho linakutoka la kutosha na iwe ni jambo la kila mara na siyo unaenda jumamosi na jumapili (weekend) tu, hiyo haitoshi, fanya mazoezi mara 4 mpaka mara 5 kwa wiki.

7. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (faiba)

Umesikia mara nyingi kwamba unahitaji kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa ajili ya kuwa na afya bora, mmeng’enyo wa chakula wenye afya na hata kukusaidia kupunguza uzito. Kile ulikuwa hujuwi pengine mpaka sasa ni kuwa vyakula hivi vyenye nyuzinyuzi ni vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu au takataka mbalimbali.

Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho, mchele wa brown (ule wanashauriwa watu wa kisukari wautumie), maharage meusi, njegele, tende, viazi vitamu, tufaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano ambao haujakobolewa.

8. Funga kula

Ndiyo, kama ulikuwa hujuwi namna nyingine rahisi ya kuondoa au kupunguza sumu mwilini ni kufunga kula kabisa kutwa nzima. Ukifunga kula mwili unalazimika kuvitumia vile vilivyomo ndani yake bila kushughulika kuvisaga vingine vipya unavyokula. Kunapokuwa hakuna shughuli ya kuvisaga na kumeng'enya chakula kipya mwilini ndipo mwili unaweza kuondoa sumu na taka nyingine kirahisi zaidi.

Amua kufunga kula kabisa kwa wiki mara 2 hata 3 ili kuondoa au kupunguza sumu, hii inaweza kuwa pia ni njia mojawapo ya kufanya maombi na kujiweka karibu na muumba wako.

Monday, March 27, 2017

MADHARA YA POMBE KIAFYA

Pombe za aina ya kinywaji ambacho kinapendwa sana katika jamii, hata hivyo licha ya kuwepo kwa taarifa ya kwamba pombe huongeza furaha ya moyo,  na kuzuia matatizo yatokanayo na msongo wa mawazo, tafiti mbalimbali zinasema ya kwamba pombe zina aina zote kemikali ambazo baadhi ya hizo kemikali huwa ni katika mwili wa mwanadamu.

Labda kwa dakika chache tuangalie matatizo yatokanayo na utumiaji wa pombe.

1;Vidonda vya tumbo.
2;Kansa ya utumbo.
3;Kusinyaa kwa Ini.
4;Kansa ya Ini.
5;Kansa ya umio(oesophagus)
6;Vindonda kwenye mapafu.
7;Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni
.Matatizo ya ganzi miguuni na mikononi(Peripheral Neuropathy).
8.Kisukari.
9;Figo kushindwa kufanya kazi.(Renal failure)
10;Kansa ya figoKukosa au upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.
(Loss of Libido)
12;Upungufu wa nguvu za kiume.
           Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa kama vile Kifua Kikuu,
   1;Kansa,
    2;KisUkari,
     3;Shinikizo la damu la kupanda.
    3;Kukosa hamu ya kula.
(Anorexia)
4; Kutovyonzwa vyema kwa chakula(Malabosorption)
Ugonjwa wa kongosho.(Pancreatis).
          Kichaa cha pombe(mtu hawezi kufanya kazi bila ya pombe,au anakuwa kama mgonjwa lakini akipewa pombe tu anakuwa mzima)
Jambo la muhimu ni kuhakikisha unaepuka utumiaji wa pombe ila kuepuka matatizo niliyoyatabainisha hapo awali.

Monday, March 20, 2017

KUWA MAKINI KATIKA KUOSHA NYWELE ZAKO


Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

Saturday, March 18, 2017

Maana ya herufi M kiganjani


Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla.

Pia inasemekana watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara.

Kama una mpenzi mwenye alama 'M' katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu.

Watu wenye herufi 'M' katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao.

Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao.

Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya 'M' basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu.

Saturday, March 11, 2017

TAmbua siri ya herufi ya mwanzo katika jina lako

Siri ya herufi ya mwanzo ya Jina lako

Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako.

>HERUFI A
>Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda.
>HERUFI B
>Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe,
>HERUFI C
>Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha,
>HERUFI D
>Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa,
>HERUFI E
>Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba,
>
>HERUFI F
>Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha Nyota ya Mashuke,
>HERUFI G
>Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha Nyota ya Mizani,
>HERUFI H
>Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha Nyota ya Nge,
>HERUFI I
>Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya Mshale,
>HERUFI J
>Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J inawakilisha Nyota ya Mbuzi,
>HERUFI K
>Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo,
>HERUFI L
>Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara. Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki,
>HERUFI M
>Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi M inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI N
>Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana. Herufi N inawakilisha Nyota ya Ngombe
>
>HERUFI O
>Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha
>HERUFI P
>Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa
>HERUFI Q
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba
>HERUFI R
>Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke
>HERUFI S
>Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani
>HERUFI T
>Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi S inawakilisha Nyota ya Nge
>HERUFI U
>Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale.
>HERUFI V
>Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mbuzi.
>HERUFI W
>Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya Ndoo.
>HERUFI X
>Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.
>HERUFI Y (YASINTA)
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI Z
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.

ZIJUE NYOTA NA TABIA ZAKE

Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia.
Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.

Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:
1. Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi
2. Kondoo (Aries): Machi 21 – Apr 19
3. Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
4. Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Ju 20
5. Kaa (Cancer): Juni 21 – Julai 22
6. Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22
7. Mashuke (Virgo):Agosti 23 – Se 22
8. Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 2
9. Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
10. Mshale (Sagittarius): Nov 22- D 21
11. Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan
12. Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 1

Makundi ya Alama za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika,

elementi 4 zijulikanazo kama:
Moto: Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
Maji: Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
Hewa: Imara na yenye kukuza a kuendeleza
Udongo: Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha

Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.

Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto: Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi

Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:
Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”:
 Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
Yenye Kubadilika “Mutable”:
Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
Isiyobadilika “Fixed”:
Mapacha Mizani, Mshale na Samaki

Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo

Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.

Haiba na Tabia za Alama za Nyota
#1 Nyota ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19
Ni mwenye maamuzi yasiyopin na mtendaji mzuri wa kazi. Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa Mwenzilishi wa mambo na mbunifu Kiongozi Muongeaji Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa. Mwaminifu kwa marafiki na familia Anajali mpenzi wake na mweny hisia kali za mapenzi

#2 Nyota ya Ng’ombe: Aprili 20 – Mei 20
Ni alama ya udongo: Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili Makini na muangalifu Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi Mstahimilivu Mwenye kutegemewa Ni mgumu kubadilika Anapenda vitu vizuri na vy thamani Unapenda urembo na vitu vya kupendeza Mwenye hisia zilizofichika Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa n mali au fedha.

#3 Nyota ya Mapacha: Mei 21 - Juni 20 
Ni alama ya hewa: Ni mwenye kipajikikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa Anafikiri kwa haraka na mches Ni mwasilianaji mzuri Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko. Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu Hana utulivu Ana mipango na malengo makubwa Mwenye kubadilika kirahisi

#4 Nyota ya Kaa: Juni 21 – Jul 22 
Ni alama ya maji: Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na ama Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo Hisia zake ni za wazi na ni rahis kujulikana Ana huruma Ni mwangalifu Mkimya na

#5 Nyota ya Simba: Julai 23 – Agosti 22
Ni alama ya moto: Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu. Anapenda kuonekana na watu Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri. Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa Ni viongozi wazuri na wenye nguvu Mwenye matumaini mazuri Mwenye kuheshimika Mshindani Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya Mwenye mvuto

#6 Nyota ya Mashuke: Agosti 23 – Septemba 22
Ni nyota yenye alama ya udongo Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja. Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu. Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao Wanajali afya

#7 Nyota ya Mizani: Septemba 23 – Oktoba 22
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro. Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili Husimamia haki na usawa Anapenda sanaa na urembo Wabunifu wa sanaa Ni mpenzi wa muziki Ni muwazi katika kuonyesha
upendo Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia Mpenda amani Wenye mvuto wa kupendwa

#8 Nyota ya Ng’e: Oktoba 23 – Novemba 21
Ni alama ya nyota ya maji na ni mwenye hisia nzito Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri Mjasiriamali namwenye uwezo kukabiliana na vizingiti vikubw Anapenda malumbano makali Wanatumia nguvu Jasiri Wastahimilivu Washindani Wanauwezo , Wachunguzi wa mambo Wasiri Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki Wanajitegemea Ni wenye maamuzi

#9 Nyota ya Mshale: Novemba 22 – Desemba 21
Ni alama ya moto na ni mwenye mapenzi mazito na vitu Mwanafalsafa na mkusanyaji  habari Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele. Ni mwenye kupenda uhuru  Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake Rafiki Mwenye ari Hawana utulivu Waaminifu na wakweli Wanapenda safari

#10 Nyota ya Mbuzi: Desemba 22 – Januari 19
Ni alama ya udongo na mwenye kuhitaji nyumba yenye amani ili kuhi ukamilifu. Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri mambo-Mtendaji Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe. Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha Mgumu kubadilika Mbishi na asiyekubari kushinda kirahisi Mfanyabiashara Mwajibikaji

#11 Nyota ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18
Ni alama ya hewa: Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria. Wakipekee Anaejitegemea na hupenda kuw peke yake Mwenye huruma Muona mbali Mwenye ufahamu wa hali ya ju nma mbunifu Anafanya marafiki wa aina mbalimbali Ana utu na mwenye kudai haki Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa harak Anapenda sanaa na maisha ya anasa.

#12 Nyota ya Samaki: Februar 19 – Machi 20
Ni alama ya maji na ni mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo. Ni mkweli na mwenye hisia nzi Hana ubinafsi Ni mpenzi mwaminifu na rafiki Mpenda amani Ana huruma Anajitoa Wana ndoto Wabunifu Wana aibu

Thursday, March 9, 2017

SULUHISHO LA UGUMBA WANAWAKE

kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake.

Ni jinsi gani nitapata ujauzito? Ni swali la kawaida kwa wanawake wengi miaka ya sasa. Ugumba ni tatizo linaloendelea kuongezeka siku kwa siku katika jamii tunayoishi sasa. Inapotokea mwanamke anamaliza miezi hata mwaka au miaka bila kupata ujauzito basi hiyo ni ishara kuna jambo mahali fulani katika mwili wake halipo sawa.

Ukweli ni kuwa wakati mwingine ugumba unaweza usiwe ndiyo chanzo cha mama huyu kutopata ujauzito bali mara nyingi mama anakuwa anakosa viinilishe mhimu na sahihi kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupata ujauzito katika mwili wake.

Nini husababisha ugumba kwa wanawake?

Mayai kutokomaa ipasavyo:
Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri.

Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema:

(1) Matatizo ya kihomoni
Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni:

Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus
Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika.
Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari

Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari.

(2) Kovu katika Ovari
Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili.

(3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause)
Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu.

Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi.

(4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari:
Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika.

Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes):
Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa.

Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo:

(A) Maaambukizi
Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema.

(B) Magonjwa yasiyo ya kawaida
Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea.

(C) Upasuaji uliopita
Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi.

(D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi:
Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha.

(E) Hali ya kurithi
Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. .

(5) Sababu za kitabia:
Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo:

Lishe na mazoezi
Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi.

Uvutaji sigara
Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake.

Unywaji pombe
Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume.

Madawa ya kulevya
Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito.

Utowaji mimba
Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara.

(6) Sababu za ugumba za kimazingira:
Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa:

Risasi (Lead)
Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion).

Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini
Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili.

Ethylene Oxide
Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage).

Dibromochloropropane (DBCP)
Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika.

(7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke:
Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi.

Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika.

Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba:

1. Chipsi
2. Vinywaji baridi
3. Kaffeina
4. Nyama nyekundu
5. Sukari
6. Soya
7. Vilevi vyote

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia

1. Pata usingizi wa kutosha kila siku
2. Epuka mfadhaiko (Stress)
3. Fanya mazoezi ya viungo kila mara
4. Kunywa maji mengi kila siku lita 2 mpaka 3