Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.
Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng'enyo wa chakula mwilini mwako.
Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:
-Uchovu sugu
-Maumivu ya maungio
-Msongamano puani
-Kuumwa kichwa kila mara
-Tumbo kujaa gesi
-Kufunga choo au kupata choo kigumu
-Kukosa utulivu
-Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
-Pumzi mbaya
-Mzunguko wa hedhi usio sawa
-Kuishiwa nguvu
-Kushindwa kupungua uzito
-Kupenda kula kula kila mara
Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini
1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee
Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi. Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee.
2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani
Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).
3. Fanya masaji
Kwa bahati mbaya waTanzania wengi hawajuwi kuwa masaji ni sehemu ya tiba au ni dawa pia kwa magonjwa mengine mengi mwilini. Wengi tunaichukulia masaji kama kitu cha starehe tu (relaxation) lakini unaweza kutumia masaji kama njia mojawapo ya kuondoa sumu mwilini na utafanikiwa kwa muda mfupi sana.
4. Kunywa maji mengi kila siku
Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni. Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.
Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo. Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo ili kusafisha damu na mwili kwa ujumla ni lazima unywe maji ya kutosha kila siku.
5. Acha chai ya rangi na Kahawa
Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa. Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai. Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake. Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).
6. Fanya mazoezi ya viungo
Inashangaza sana kuona waTanzania wengi hawaoni umhimu wa kufanya mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo ni jambo la lazima kama ilivyo chakula. Iwe unaumwa au huumwi, iwe una uzito kuzidi au una uzito wa kawaida hakikisha unapata muda wa kufanya mazoezi.
Mazoezi yanakusaidia kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kukuondolea mfadhaiko au stress kirahisi zaidi, sambamba na hilo mazoezi ni dawa tosha na nzuri ya kuondoa sumu mwilini haraka zaidi. Hakikisha jasho linakutoka la kutosha na iwe ni jambo la kila mara na siyo unaenda jumamosi na jumapili (weekend) tu, hiyo haitoshi, fanya mazoezi mara 4 mpaka mara 5 kwa wiki.
7. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (faiba)
Umesikia mara nyingi kwamba unahitaji kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa ajili ya kuwa na afya bora, mmeng’enyo wa chakula wenye afya na hata kukusaidia kupunguza uzito. Kile ulikuwa hujuwi pengine mpaka sasa ni kuwa vyakula hivi vyenye nyuzinyuzi ni vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu au takataka mbalimbali.
Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho, mchele wa brown (ule wanashauriwa watu wa kisukari wautumie), maharage meusi, njegele, tende, viazi vitamu, tufaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano ambao haujakobolewa.
8. Funga kula
Ndiyo, kama ulikuwa hujuwi namna nyingine rahisi ya kuondoa au kupunguza sumu mwilini ni kufunga kula kabisa kutwa nzima. Ukifunga kula mwili unalazimika kuvitumia vile vilivyomo ndani yake bila kushughulika kuvisaga vingine vipya unavyokula. Kunapokuwa hakuna shughuli ya kuvisaga na kumeng'enya chakula kipya mwilini ndipo mwili unaweza kuondoa sumu na taka nyingine kirahisi zaidi.
Amua kufunga kula kabisa kwa wiki mara 2 hata 3 ili kuondoa au kupunguza sumu, hii inaweza kuwa pia ni njia mojawapo ya kufanya maombi na kujiweka karibu na muumba wako.
No comments:
Post a Comment