Wednesday, October 5, 2016

MALENGO NA MAONO YETU .

*BINADAMU ASIYEKUWA NA
MAONO HUPOTEA*

*_Relax and trust the timing of your life, you will figure out your career, you will find the right relationship, you will become The person you always wanted to be, Just don't forget to appreciate who you are now_*

Maono ni nini, ili kufahamu vizuri dhana nzima ya maono ni kujiuliza swali moja *UNATAKA UKUMBUKWE KWA JAMBO GANI* kimsingi unataka kuleta tofauti gani katika hii dunia.

Nini unakiona kwenye maisha yako miaka michache ijayo, unapanga kufanya nini kwa muda mrefu wa maisha yako.

Akili yako imebeba picha ya aina gani? Picha hiyo ndiyo inayotengeneza maisha yako, inatengeneza kuamua kwako, kuongea kwako, mavazi yako, kazi unayoifanya, marafiki uliyo nao. Nk
👆👆👆👆👆
Vyote hivi vinajengwa na taswira uliyo Nayo wewe mwenyewe juu ya maisha yako katika akili yako.

Sasa kumbe maono yanatupa faida zifuatazo.

Thought 1
*uwezo wako wa kuamua na kutendea kazi mawazo yako vinategemea kiwango chako cha kuamini juu ya taswira uliyo nayo kuhusu maisha yako*

Thought 2.
*kiwango chako cha maisha kinapimwa na kiwango cha maono yako, ukiwa na maono madogo jua na maisha yako yatakuwa ya kawaida*

Thought 3
*Maono yanaondoa uvivu na kukata tamaa kwasababu mtu anaejua anakokwenda ni vigumu sanaa kumzuia*

Thought 4
*maono yanatabia ya kumjengea muhusika Hamu ya kutafuta taarifa hasa kuhusu ono lake, lakini pia kumpaa maarifa ya namna ya kuwekeza kwenye maono yake*

Ukisha tambua unataka kufika wapi katika maisha yako, hakikisha hakuna mtu yoyote anaekukatisha tamaa.
👆👆👆👆👆👆
Kuanzia Leo anza kuamini kwamba maono yako yanaweza kutimia, anza kuamini mawazo yako na Mapito yako kwamba ndivyo vitakavyo kufikisha mahali unapo pataka.

Nb
*_The key to a positive life is to focus on the solution not the problems_*

*_one day all the people that did not believe in you, Will tell every one how they meet you_*

Napenda kukuona ndg yangu tukiwa tumefanikiwa na kufikia malengo yetu kila siku kwa kulifanya kwa kiasi chake
.  
MUNGU YU PAMOJA NASI DAIMA KATIKA KILA LILILO  MBELE YETU.
  BY MR B.MWAMPULULE

No comments:

Post a Comment