Habari za asubuhi ndg jamaa na rafiki yangu natumaini kwa uweza wa mwenyezi MUNGU u mzma wa afya njema .
Naomba siku ya Leo tuendelee kutambua namna gan ya kuona fursa zituzungukazo katika jamii zetu .
Tambua ya kwamba tunaposema neno fursa imesheheni vitu ving ndan yake.sasa tuangalie baadhi ya fursa zinazotuzunguka.
1:endapo tupo katika jamii ambayo iko katika mazingira ya vijijini .
Hapo kuna fursa nying sana ambapo kupitia maisha ya kijijini kuna baadhi ya mahitaji muhimu sana ambayo huhitajika katika maisha yetu ya kila siku.
Sasa hapa napenda nikutajie fursa kama ifuatayo kama ni sehemu isiyo na umeme
1;uuzaji wa mafuta ya taa
2;uuzaji wa taa za mafuta ya taa
3;uuzaji wa taa za sola
4:uuzaji wa majiko ya mafuta (ya mchina)
5;uuzaji wa tambi za taa na majiko n.k
Pia kuna fursa nying sana ambayo unaweza kuziona hizo ni baadhi tu.
Kumbuka tatizo linaloikumba jamii kwa kiasi kikubwa hiyo ni fursa na pia hiyo ni changamoto kubwa sana ambapo huwa inahitajika Mara kwa Mara katika jamii kama mahitaji muhimu katika jamii.
Kwa Mara nyingne ukiweza kutatua hilo tatizo utasababiasha kuanza kupendwa sana na jamii na kuwa t ayari ni msaada kwao kwa mana umeweza kuwasogezea huduma za muhimu karibu Yao.
Kwa Leo tuishie hapa lakn muda ujao tunaendelea tena kutambua fursa ambazo bado tuko nazo katika jamii.
Kwa mabadiliko ya fikra na maendeleo daima tuendelee kupitia ukurasa wetu kwa ajili ya kutambua mambo mbalimbali na pia ukijaribu kuongeza na vingne uvionavyo katika jamii yako.
Asante sana nakutakia siku njema .
By Mr B mwampulule.
No comments:
Post a Comment