Habari za Leo ndg jamaa na marafiki zangu .natumai wote mu wazma wa afya kwa uwezo wa MUNGU. Kwa maana yy ndio mwenye uweza wa kutupatia vyote tulivyonavyo .
Ndg yangu siku ya Leo napenda tukumbushane kitu kimoja ambacho ni muhimu sana kukitambua katika maisha yetu ambacho hicho kitu ni THAMANI YAKO YA KUWEPO DUNIANI.
Naomba nikuulize kitu kimoja ewe ndg yangu .je hapo ulipo umewahi kujiuliza ni wangapi uliishi nao ulikuwa nao na kwa sasa hawapo tena?
Na pia umewahi kujiuliza ni kwa nn ww uwepo hai mpaka muda huu ?
TAMBUA ya kwamba hapo ulipo ww na hapa nilipo mm ni kwa neema na rehema za mwenyezi MUNGU .
Na pia tambua ya kwamba kuwepo kwako hapo kuna jambo kubwa sana lililopo mbele yako ambalo ni jukumu na wajibu wako wa kuweza kulifanikisha katika uhai wako.
Daima thamani yako ww na mm ni kubwa sana kwa mwenyezi MUNGU ambapo MUNGU katupa nafasi nyingne kwa ajili ya kukamilisha lile jambo lililo la muhimu kwako ambalo mwingne hana ili ulikamilishe na jamii ifaidike kutokana na hilo jukumu lako ndg yangu.
Kila siku ziendavyo ndivyo unavyozidi kuona ya kwamba ni jukumu gan lilivyo mbele yako lililo na manufaa kwako na jamii nzima.
Ndugu yangu naomba tutambue thamani zetu kila siku.
Napenda kuona tukizd kufanikiwa katika malengo yetu ndg yangu .
MUNGU YU PAMOJA NASI DAIMA TUKAZE BUTI TUTAFIKA.
BY MR B.MWAMPULULE
No comments:
Post a Comment