Friday, April 7, 2017

HISTORIA YA SHEIKH ABEID KARUME

Mnamo tarehe 7 Aprili, 1972 Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui mjini Zanzibar. Katika mfululizo wa makala haya mwandishi.

Bwana Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu). Bwana Amani Karume na Bibi Amina Binti Kadudu walifunga ndoa huko Mwera.

Bwana Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu wanne wa baba mmoja na mama mmoja ambao ni wanaume wawili na wanawake wawili. Lakini wote walifariki kutokana na maradhi mbalimbali na kubaki yeye peke yake. Kwa upande wa mama mmoja, Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja ambao ni Asha, Shumbana na Othman. Baba yake mzazi Abeid Amani Karume alifariki dunia mwaka 1909 wakati Abeid Amani Karume akiwa na umri wa miaka minne. Bwana Abeid Amani Karume alipata elimu ya Kurani na alianza masomo ya msingi katika skuli ya Mwera mwaka alofariki baba yake wa 1909, ambapo darasa lao lilikuwa la kwanza kuifungua skuli hiyo.

Katika mwaka 1913 wakati akiwa na umri wa miaka 8 mama yake mzazi alimpeleka mjini Unguja kuendelea na masomo. Huko aliishi na mjomba wake aliyekuwa Sajenti katika jeshi la polisi la King African Rifle (KAR). Kwa bahati mbaya muda wake wote wa masomo ulikuwa miaka mitatu. Akiwa mjini Zanzibar Abeid Karume alipata marafiki kadhaa na kuvutiwa mno na harakati za bandari ya Zanzibar.

Kwa wakati huo, bandari ya Zanzibar ndiyo iliyokuwa kubwa Afrika mashariki. Pia Zanzibar, ilikuwa ndiyo kituo kikuu cha biashara katika eneo zima la Afrika mashariki na Maziwa Makuu.

Meli za mataifa ya nje hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia zilitia nanga bandarini Zanzibar kupakia na kupakua bidhaaa mbalimbali. Pia meli nyingi zilifika Zanzibar kuchukua maji safi ya kunywa yatokayo katika chemchem ya Mwanyanya. Meli hizo zilitoa ajira ya muda ya kusafisha mashine na kupangusa moshi. Mara nyingi mabaharia wa meli hizo waliajiri watoto kuwachukulia vikapu vya kununulia vyakula sokoni na kuwalipa ujira mdogo.

Kwa vile alipendelea kazi ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifuatana na bwana mmoja aitwae Juma hadi bandarini. Alijumuika na watoto kadhaa waliofuata ajira ya muda huko bandarini. Ajira ya muda aliyoipata Karume huko bandarini ilimfanya akutane na mabaharia wa nchi mbalimbali na hivyo kuvutiwa na uzuri wa maisha ya ubaharia ya kusafiri na kuona nchi na watu mbalimbali. Hali hiyo ilimfanya Karume azidi hamu na ari ya kutafuta kazi ya ubaharia na kumuomba mama yake ruhusa ya kufanya kazi melini. Mwanzoni mama yake mzazi alikataa shauri hilo. Lakini baadaye alikubali ombi hilo baada ya kufahamishwa kuwa meli atakayofanyakazi mwanawe haitosafiri mbali na itatia nanga bandarini Zanzibar mara kwa mara.

Katika mwaka 1919 Abeid Amani Karume alipeleka barua ya kuomba kazi melini lakini alikataliwa kwa vile alikuwa na umri mdogo wa miaka 14. Hata hivyo hakuvunjika moyo na hakurudi Mwera kwa mama yake bali alimtembelea mara kwa mara. Alijiunga na timu za masumbwi na mpira wa miguu na kujuana na watu mbalimbali.

Kwa wakati huo timu za mpira wa miguu zilizojulikana Unguja zilikuwa ni timu ya skuli ya Kiungani iliyoanzishwa na Mwalimu Augostino Ramadhani na John Majaliwa. Mara nyingi timu hiyo ilishindana na timu ya watumishi serikalini. Baadaye kuliundwa timu nyengine za mpira wa miguu ambazo ni Vuga Boys, New Generation, United Service na New Kings. Karume alijiunga na timu ya New Generation na kucheza nafasi ya mstari wa mbele kushoto Inside left. Baadhi ya waanzilishi wa timu hiyo ni Bwana Malingumu, Shaaban Feruzi, Saad Shoka, Masoud Thani na Mzee wa Shangani.

Mara tu baada ya kujiunga na timu hiyo, Karume alichaguliwa kuwa msaidizi nahodha. Katika mwaka 1920 Abeid Amani Karume alikubaliwa kuwa baharia katika meli iliyoitwa Golden Crown (Taji la Dhahabu). Meli hiyo ilichukua abiria na mizigo kati ya bandari ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pemba, Tanga, Mombasa na Mikindani huko Kilwa.

Baadaye alishuka katika meli hiyo na kufanya kazi katika meli nyengine iliyoitwa Cheko. Kwa bahati mbaya, meli hiyo iligonga mwamba na kuvunjika huko Kimbiji, nje kidogo ya Dar es Salaam lakini watu wote walinusurika.

Kazi ya ubaharia ilimpa tija Abeid Amani Karume kwani alinunua nyumba na viwanja kila alipopata nafasi ya kwenda nyumbani. Kwa muda wote huo Abeid Amani Karume alifanyakazi katika meli zilizopata leseni ya kufanyakazi katika mwambao wa Afrika Mashariki.

Katika mwaka 1922, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Abeid Amani Karume alipata kazi katika meli ya kampuni ya British Indian Steam Navigation Company ya Uingereza. Akiwa na kampuni hiyo Karume, alikaa nje miaka mitatu hadi 1925, aliporejea nyumbani kwa mapumziko.Tayari wakati huo, Karume alikwishatembelea nchi za Japan,Comoro,Madagascar,China,Singapore,New Zealand,Uingereza,Marekani,
Canada,Ufaransa, Ubelgiji, India,Ureno,Hispania,Arabuni,Italia na Ugiriki.

Baada ya kupumzika kwa muda, Abeid Amani Karume alijiunga na kampuni ya Eastern Telegraph Company na kufanya kazi katika meli ya kampuni hiyo iitwayo Caranja. Meli hiyo ilikuwa ikitandika waya za simu baharini kati ya Zanzibar na Aden. Aliendelea na kazi ya ubaharia hadi mwaka 1938 alipoacha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Karume alishauriwa na mama yake mzazi kuacha kazi hiyo. Vilevile aliacha kazi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama duniani. Wakati huo, tayari vita vikuu vya pili vya dunia vilikaribia. Baadhi ya kazi alizofanya katika meli hizo ni Greaser, Fireman, Sailor na Headsailor.

Katika kipindi fulani cha kazi yake ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifanyakazi chombo kimoja na Khamis Heri Ayemba kutoka Tanga. Wote wawili walirudi nyumbani wakati vita vya pili vya dunia vinakaribia. Baada ya kuacha kazi hiyo,Khamis Heri Ayemba alijihusisha na biashara huko kwao Tanga na kuwa tajiri mkubwa. Wakati wa kudai uhuru, Ayemba alishirikiana na Peter Muhando na Mwalimu Kihere kuunda tawi la TANU huko Tanga. Tarehe 23 Oktoba, 1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wa chama hicho. Katika uchaguzi huo, Khamis Heri Ayemba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Peter Muhando alichaguliwa kuwa katibu.

Kutokana na kusafiri sehemu mbalimbali duniani, Abeid Amani Karume alijifunza mengi ya kimaisha na kuona jinsi gani mataifa ya ulaya na mabepari walivyotumia hila na ujanja kuzinyonya nchi za Afrika. Katika safari zake za ubaharia alikumbana na matatizo kadhaa. Tatizo kubwa zaidi alokumbana nalo ni dhoruba kali sana iliyoikumba meli yao wakati wakitokea Australia kwenda Lorence Marques (Msumbiji).

Katika miaka ya 1930, timu za mpira wa miguu Zanzibar zilikabiliwa na mgawanyiko. Kutokana na mgawanyiko huo, ndipo hapo mwaka 1931 timu zote za New Kings, Vuga Boys, United Service na New Generation zilipoungana na kuunda umoja wa michezo wa waafrika uloitwa "African Sports Club". Timu hiyo ilikuwa na "A" na "B", ambapo Karume alikuwa timu "A" iliyokuwa ya kwanza mwaka huo kwenda Tanganyika kucheza mechi ya kirafiki.

Umoja huo haukwishia hapo kwani katika mwaka 1934 uliundwa umoja wa Waafrika (African Association). Umoja huo wa Waafrika ndiyo ulogeuka kutoka kwenye michezo na kuwa umoja wa kisiasa.

Katika mwaka 1938 bandarini Zanzibar palikuwa na vijana wa Kiafrika walounda umoja uliyoitwa “Motorboats Association”. Vijana hao walikuwa wakivusha abiria kutoka bandarini hadi melini kwa kutumia mashua, kazi ambayo iliwasaidia kupata pesa chache za kuendeshea maisha. Lakini baadaye walijitokeza wafanyabiashara wajanja wenye asili ya Asia wenye uwezo na kununua boti za mashine na kuvusha abiria. Wafanyabiashara hao, walitumia mbinu ya kuungana na waafrika katika biashara hiyo.

Baada ya muda mfupi wafanyabiashara hao wenye asili ya Asia waliunda chama chao kilichoitwa Syndicate. Taratibu wafanyabiashara hao waliwaingiza ndugu zao na wale waafrika waanzilishi waligeuzwa vibarua na kulipwa ujira mdogo sana. Abeid Karume aliwakusanya waafrika hao kudai haki zao na kufanikiwa kufanya mapatano na waasia hao. Wamiliki wa maboti hao, walikubali kuwalipa waafrika asimilia 40% ya mapato yote na wao walichukua asilimia 60% na kugharamia uendeshaji na matengenezo ya boti hizo.

Baada ya mafanikio hayo Abeid Amani Karume alipata sifa nyingi na mwaka 1939 alianzisha harakati za kuunda chama cha mabaharia Zanzibar ili kupigania haki za wafanyakazi hao. Kwa wakati huo ilikuwa vigumu sana kuwashawishi watu wasojua mipango ya vyama vya wafanyakazi. Hivyo basi mwishoni mwa mwaka huo wa 1939 baadhi ya wafanyakazi waloshauriwa kuanzisha umoja huo walikataa kushiriki katika umoja huo. Karume hakusita na juhudi zake za kuanzisha umoja huo. Mwaka huohuo wa 1939, alionana na mzungu aitwae Bwana Douglas Basil Berber aliyekuwa Inspekta wa polisi kuomba kibali cha kuanzisha chama cha mabaharia wa Unguja na Pemba.

Mzungu huyo alimshauri Abeid Karume awakusanye wale wote wanaotaka kuanzisha chama hicho na wajiunge kwa mujibu wa sheria za India. Zanzibar kwa wakati huo haikuwa na sheria kuhusu vyama vya wafanyakazi Waafrika.

Baada ya kuwashauri wenzake, Abeid Karume alipata watu sita walokubali kujiunga na jumuiya hiyo. Watu hao ni Bakari Jabu, Miraji Mselem, Juma Maalim, Ismail Mbarouk, Mbarouk Salim na Kitwana Suwedi. Chama cha Mabaharia wa Unguja na Pemba kilipata usajili tarehe 30 Ogosti, 1949 na Makao Makuu yake yalikuwa Kisima majongoo.

Sheria ya vyama vya wafanyakazi vya Zanzibar ilipitishwa mwaka 1931. Baadaye katika mwaka 1941, sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko na kuwa Sheria Nambari 3 ya vyama vya wafanyakazi.

Jumuiya za mwanzo za wafanyakazi kuanzishwa Zanzibar ni pamoja na Jumuiya ya Mabaharia, Jumuiya ya Wachukuzi na Umoja wa Watumishi wa Majumba ya Wazungu. Hadi kufika mwaka 1951 tayari chama cha mabaharia kilikuwa na wanachama 83. Tarehe 26 Oktoba 1959, Abeid Karume ambaye ni muasisi wa jumuiya ya mabaharia aliacha uongozi wa jumuiya hiyo na kujihusisha zaidi na siasa katika chama cha ASP ,lakini aliendelea kuwa mdhamini wa jumuiya hiyo. Kabla ya hapo katika mwaka 1942, Karume alikuwa katibu wa African Association na Rais wa Jumuiya hiyo hapo mwaka 1953. Baadaye nafasi hiyo ilishikiliwa na Bwana Herbert Barnabas.

Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini.

Bibi Fatma Gulamhussein Ismail alizaliwa Bumbwini mwaka 1929 akiwa ni mtoto wa Bwana Gulamhussein Ismail na Bibi Mwanasha Mbwana Ramadhani. Wazazi wa Bibi Fatma Karume ni wazaliwa wa Bumbwini. Bi Fatma Karume alipata elimu ya msingi katika skuli ya Bumbwini na kuolewa mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo hayo. Mara tu baada ya kufunga ndoa, Bibi Fatma Karume na Bwana Abeid Amani Karume walihamia mtaa wa Kisimamajongoo nyumba Nambari 18/22 mjini Unguja kwa Sheikh Karume. Nyumba nyengine mbili za Bwana Karume zilikuwa Gongoni na Michenzani.

Bi.Fatuma Karume alijifungua mtoto wa kwanza wa kike aliyeitwa Asha katika mwaka 1946, lakini mtoto huyo alifariki siku ya pili yake. Mtoto wa pili wa hayati Karume ni Amani Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 1 Novemba, 1948. Mtoto wake wa tatu ni Ali Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 24 Mei, 1950.

Mama yake mzazi Abeid Amani Karume, Bibi Amina binti Kadudu alifariki dunia 1963 na kuzikwa katika makaburi ya Michenzani. Wake wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.

Mbali ya kuanzisha chama cha mabaharia pia Abeid Amani Karume alikuwa muasisi wa Jumuiya ya Waafrika iliyoitwa African Dancing Club katika mwaka 1940. Jumuiya hiyo ilikuwa na lengo la kuwaunganisha pamoja vijana wa African Association.

Rais wa Jumuiya hiyo ya "African Dancing Club" alikuwa ni Bwana Pearcy Baraka, Abeid Karume alikuwa Katibu Mkuu na Mweka hazina ni Mtumwa Zaidi. Mbali ya kumiliki bendi ya muziki vilevile African Dancing Club ilinunua banda la zamani ambalo lilibomolewa na kujengwa makao makuu. Baadaye hapo tarehe 31 Januari, 1949 “African Dancing Club” ilibadilishwa jina na kuitwa “African Youth Union”.

Kuundwa kwa chama cha Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) mapema katika miaka ya 50 na kutolewa kwa mapendekezo ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar katika mwaka 1957 yaliwafanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika African Association, na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana. Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo basi Jumuiya ya Shirazi Association ilimtuma Bwana Haji Khatibu aliyekuwa rafiki mkubwa wa Abeid Amani Karume apeleke shauri la kuunganishwa Jumuiya ya Waafrika na Jumuiya ya Washirazi.

Kabla ya kukutana, kila jumuiya ilifanya kikao cha faragha kujadili agenda ya mkutano. Shirazi Association walikubaliana kupendekeza jina la Abeid Karume kutoka African Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa.

Nao African Association, walipanga kupendekeza jina la Sheikh Ameir Tajo kutoka Shirazi Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa. Viongozi wa Jumuiya hizo walikubaliana kukutana kuanzia tarehe 1 hadi 5 Februari,1957. Mkutano ulifanyika kama ulivyopangwa hapo Mwembe Kisonge nyumbani kwa Abeid Amani Karume chini ya Mwenyekiti wake Muhidini Ali Omar. Kwa wakati huo, nyumba hiyo ya Abeid Karume alikuwa aliishi Hija Saleh na Haji Ali Mnoga.

Mkutano huo ulimalizika jioni ya tarehe 5 Februari, 1957 kwa viongozi hao kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association na kuunda chama kilichoitwa Afro - Shirazi Union.

Baadaye chama hicho kiliitwa Afro - Shirazi Party, jina ambalo lilitolewa na Ali Khamis kutoka Shirazi Association. Viongozi 18 wa African Association na Shirazi Association walikutana na kuunda Afro -Shirazi Party. Kumi ni kutoka African Association na Wanane kutoka Shirazi Association. Viongozi wa African Association walikuwa ni Abeid Amani Karume, Ibrahim Saadala, Abdalla Kassim Hanga, Bakari Jabu, Mtoro Rehani Kingo, Rajabu Swedi, Ali Juma Seif, Mtumwa Borafia, Saleh Juma na Saleh Mapete. Viongozi wa Shirazi Association ni Thabit Kombo Jecha, Muhidini Ali Omar, Ameir Tajo, Ali Khamis, Haji Khatibu, Mdungi Ussi, Ali Ameir na Othman Sharifu.

Katika mkutano huo pia alikuwepo mgeni mwalikwa Rais wa TANU, Mwalimu J.K. Nyerere na Katibu Mkuu wa chama cha TANU, Bwana Zubeir Mtemvu. Pia alihudhuria Bibi Maida Springer Kemp ambaye ni Mmarekani mweusi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Viwanda wa Marekani American Federation of Labour Congress of Industrial Organization AFL - C 10. Bibi Springer alikuwa ziarani barani Afrika kuangalia harakati za ukombozi na alifuatana na Mwalimu Nyerere aliyepitia Zanzibar akielekea Tanga kuitangaza TANU.

Chama cha Afro - Shirazi Party kilimteuwa Abeid Amani Karume kuwa Rais, Mtoro Rehani Kingo kuwa Makamo na Thabit Kombo Jecha ni Katibu Mkuu. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ni Ibrahim Saadala, Ali Khamis, Ameir Tajo, Mtumwa Borafia na Muhidini Ali Omar. Baadaye wajumbe wa Shirazi Association kutoka Pemba ambao ni Muhamed Shamte, Ali Sharif Mussa, Issa Sharif, Suleiman Ameir na Hassan Ali waliitwa na kufahamishwa juu ya kuunganishwa vyama hivyo.

Katika mwaka 1947 kuliundwa serikali za mitaa (Local Government) na Baraza la Manispaa (Township Council) lilianzishwa 1954. Abeid Karume alichaguliwa kuwa diwani (Councillor). Katika mwezi wa Juni 1957, Bwana Karume alikwenda nchini Ghana kuhudhuria sherehe za uhuru wa taifa hilo. Safari hiyo ilikuwa ni mwaliko wa kiongozi wa nchi hiyo, Bwana Kwameh Nkrumah kwa vyama vyote vya kupigania uhuru barani Afrika.

Abeid Amani Karume alipendekezwa na chama cha ASP kuwa mgombea wa kiti cha baraza la kutunga sheria wa jimbo la Ng'ambo, katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar wa 1957. Katika uchaguzi huo, Abeid Amani Karume alijiandikisha katika jimbo la Ng'ambo kituo Nambari 84 ambacho ni Old Shimoni School (Mao tse Tung) akiwa ni mfanyabiashara, mkaazi wa Kisima Majongoo nyumba Nambari 18/22. Kadi yake ya kupigia kura ilikuwa Nambari 5818. Karume alishinda kiti hicho kwa kura 3,328 dhidi ya wapinzani wake Ali bin Muhsin Barwan wa ZNP aliyepata kura 918 na Ibuni Saleh mgombea binafsi aliyepata kura 55.

Miaka 40 iliyopita hapo tarehe 7 Aprili, 1972 Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui mjini Zanzibar. Katika mfululizo wa makala haya mwandishi Ali Shaaban Juma anaelezea historia ya maisha ya Mwanamapinduzi huyo.

Hapo tarehe 15 Januari, 1960 Abeid Karume alishtakiwa na mfanyabiashara aitwae Punja Kara Haji mkaazi wa Darajani mjini Unguja. Karume alishtakiwa kwa madai ya kuvunja mkataba wa kukodi bekari ya mfanyabiashara huyo.

Kesi hiyo Nambari 4 ya 1960 (Civil Case Number 4 of 1960) ilitayarishwa na wakili Dinshaw Karai kwa niaba ya Punja Kara Haji. Ilidaiwa mbele ya Jaji G.J. Horsfall wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kuwa hapo tarehe 17 Aprili,1958, Abeid Karume na Thabit Kombo waliingia mkataba na Punja Kara Haji wa kukodi bekari ya Mchangani, nyumba nambari 2759 mali ya Punja Kara Haji.

Mkataba huo ulieleza kuwa kodi hiyo itakuwa ni ya miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Mei 1958 kwa malipo ya Shilingi 7,395/20. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 550/- kila mwezi. Waraka wa makubaliano hayo ulotayarishwa na Wakili Dinshaw Karai ulitiwa saini hapo tarehe 18 Novemba, 1959 na Punja Kara Haji kwa niaba yake na Abeid Karume kwa niaba yake na kwa niaba ya Thabit Kombo. Mkataba huo ulishuhudiwa na mawakili Dinshaw Karai na Hemed Said.

Akiwasilisha madai dhidi ya Karume hapo tarehe 27 Januari, 1960 Punja Kara Haji alidai kuwa tarehe 16 Novemba, 1959 Abeid Karume alifika nyumbani kwake na kumueleza kuwa yeye na Thabit Kombo wanataka kuiacha bekari hiyo kwa vile ilikuwa inawatia hasara.

Punja Kara Haji alieleza mahakama hiyo kuwa, baada ya kupata kauli hiyo ya Abeid Karume walifikia makubaliano na mlalamikiwa. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 7,395/20 kama ilivyo katika mkataba wao wa tarehe 17 Aprili, 1958. Pia Karume alitakiwa akabidhi jengo la bekari hiyo kwa mwenyewe hapo tarehe 31 Disemba, 1959. Akiendelea kutoa ushahidi wake Punja Kara Haji alidai mahakamani kuwa yeye na Karume walikubaliana fedha hizo Shilingi 7,395/20 zilipwe kwa awamu kwa udhibitisho wa maandishi.

Awamu ya kwanza ya Shilingi 2,000/- ziwe zimelipwa ifikapo Disemba, 1959. Fedha zilizobaki Shilingi 5,395/20 zilipwe kidogo kidogo kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi kuanzia tarehe 1 Januari, 1960. Fedha hizo zilitakiwa ziendelee kulipwa kwa utaratibu huo kila siku ya mwanzo ya kila mwezi. Punja Kara alidai kuwa Abeid Karume alishindwa kulipa Shilingi 2,000/- hapo tarehe 1 Disemba,1959 na hakulipa Shilingi 500/-ilipofika tarehe 1 Januari,1960 kama walivyokubaliana. Kutokana na madai yake hayo, Punja Kara Haji alidai mahakamani alipwe na Abeid Karume Shilingi 7,395/20, asilimia 9% ya riba ya mwaka kuanzia tarehe ya hukumu na alipwe gharama za kesi hiyo.

Waraka ulomtaka Abeid Karume kufika mahakamani tarehe 8 Februari, 1960 saa 3.00 asubuhi ulitiwa saini na Mrajisi wa mahakama Hussein A. Rahim tarehe 27 Januari, 1960.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo Abeid Karume aliambia mahakama hiyo kuwa hapo tarehe 20 Januari, 1960 alimlipa Punja Kara Haji Shilingi 1,000/-. Pia walikubaliana kuwa deni lililobaki lilipwe kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi. Karume alieleza kuwa licha ya makubaliano hayo, mlalamikaji alifungua mashtaka hapo tarehe 27 Januari,1960 bila kutoa stakabadhi ya malipo ya Shilingi 1000/- alizopewa. Baada ya kupokea waraka wa kumtaka afike mahakamani kujibu kesi hiyo,Karume alikwenda kwa Punja Kara Haji ambaye alimweleza Karume kuwa mashtaka dhidi yake yalifunguliwa na wakili wake aitwae Dinshaw Karai baada ya kutofahamiana na mteja wake .

Punja alimuhakikishia Abeid Karume kuwa atamwambia wakili huyo aifute kesi hiyo mara moja. Abeid Karume alieleza mahakama hiyo kuwa, kwa vile aliyaamini maneno ya Punja hakuona ulazima wa kufika mahakamani kujibu kesi hiyo. Inaelekea mlalamikaji (Punja Kara Haji) alitumia fursa ya kutofika Karume mahakamani na kupata upendeleo wa kisheria kwa vile kesi hiyo ilisikilizwa upande wa mlalamikaji pekee. Hivyo moja kwa moja Punja Kara alidanganya mahakama kuwa Abeid Karume alilipa Shilingi Elfu moja baada ya kufunguliwa mashtaka. Karume alieleza mahakama hiyo kuwa vile vile hapo tarehe 7 Machi, 1960 alitoa mahakamani amana ya Shilingi 2,000/- taslimu na kupatiwa stakabadhi ya malipo yenye Nambari 153/60. Lakini licha ya ukweli huo mlalamikaji aliomba mahakama hapo tarehe 11 Machi, 1960 itoe uwamuzi wa kesi hiyo. Hata hivyo Abeid Karume alishinda kesi hiyo na madai ya mlalamikaji yalitupiliwa mbali.

Katika mwezi wa Oktoba 1960, Sheikh Abeid Amani Karume alihudhuria mkutano mkuu wa chama cha Malawi Congress Party huko Nkhota Kota katika Wilaya ya kati ya Nyasaland (Malawi) akiwakilisha chama cha Afro- Shirazi. Katika mkutano huo wanasiasa wanane wa mwisho wa Malawi walokuwa kizuizini waliachiliwa huru. Wanasiasa hao walitiwa ndani kwa kupinga mpango wa wakoloni wa kiingereza wa kuanzisha Shirikisho la Rhodesia (Zimbabwe) na Nyasaland (Malawi). Baada ya kuachiliwa huru, walikabidhiwa kwa kiongozi wa chama cha Malawi Congress Party, Dr. Kamuzu Banda. Aliyewakabidhi wanasiasa hao kwa Dr.Banda ni Gavana wa mwisho wa Uingereza katika koloni la Nyasaland. Msamaha huo ulitolewa muda mfupi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru.

Wanasiasa waloachiliwa ni pamoja na Masauko Chipembere, Matupi Mkandawire, Chimtambi na wengineo. Mkutano huo wa chama cha Malawi Congress Party ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Malawi. Viongozi kadhaa wa kisiasa wa Jumuiya ya PAFMECA (Pan African Freedom Movement for East and Central Africa) walialikwa ambapo viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo walihudhuria mkutano huo.

Mbali ya Abeid Karume na ujumbe wake wa chama cha Afro -Shirazi kutoka Zanzibar, pia walihudhuria Marton Malianga wa chama cha Southern Rhodesia African National Congress cha Rhodesia (Zimbabwe) kilichoongozwa na Joshua Nkhomo. Wengine ni Namilando Mundia wa chama cha Zambia National Congress kilichongozwa na Kenneth Kaunda, Sheikh Amri Abeid Kaluta na Austin Shaba wa chama cha Tanganyika African National Union, TANU cha Tanganyika.

Vilevile alihudhuria Abdulrahman Babu na ujumbe wake wa chama cha ZNP cha Zanzibar. Kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya chama cha ASP na chama cha Malawi Congress Party cha Malawi, Abeid Karume aliwaalika kuitembelea Zanzibar baadhi ya viongozi wa chama hicho cha Malawi mapema mwaka 1965. Viongozi walotembelea Zanzibar kutoka Malawi ni Orton Chingolo Chirwa, Yatuta Chisiza, Willie Chokani, Augustine Bwanausi na Kanyama Chiume.

Abeid Karume alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria katika uchaguzi wa pili wa Januari, 1961, katika jimbo la Jang'ombe kwa tiketi ya ASP.

Mara tu baada ya kumalizika uchaguzi huo wa 1961 ulokuwa na utatanishi Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Waziri wa Afya na Mambo ya Kienyeji katika serikali ya pamoja ya miezi sita. Uchaguzi Mkuu wa tatu wa Zanzibar ulifanyika tarehe 1 Juni, 1963.

Karume alichaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria katika jimbo la Kwahani na Jang'ombe. Akiwa Waziri wa Afya, Karume alishughulikia Afya, Ajira, Ujenzi wa Nyumba, Serikali za Mitaa na Serikali za Wilaya.

Baada ya kuundwa serikali ya Waziri Mkuu Muhammed Shamte kufuatia uchaguzi wa 1963, Abeid Amani Karume aliteuliwa kuwa kiongozi wa upinzani katika baraza la kutunga sheria.

Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne walotayarisha Mapinduzi hayo kwa siri. Akiwa na umri wa miaka 59, Karume aliongoza Mapinduzi ya 1964 na alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana hapo tarehe 26 Aprili,1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 27Aprili,1964.

Akiwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Abeid Amani Karume aliongoza ujumbe wa watu kumi na tisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutembelea mikoa ya Musoma, Mwanza na Bukoba kuanzia tarehe 5 -15 Septemba,1965. Lengo la ziara hiyo ni kuonana na wananchi wa mikoa hiyo na kuwahamasisha kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Septemba, 1965.

Mheshimiwa Karume aliteuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania kupitia viti maalum vya kuteuliwa na Rais wa Tanzania. Karume alikuwa ni mmoja kati ya wabunge 23 wa kuteuliwa kutoka Zanzibar kama ilivyokuwa katiba ya wakati huo. Aliapishwa rasmi kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania katika ukumbi wa Arnatoghly mjini Dar es Salaam hapo tarehe 30 Septemba, 1965.

Katika mwezi wa Aprili 1967, Mzee Karume akifuatana na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere na wajumbe kadhaa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Tanzania walikwenda nchini Misri kuhudhuria mkutano wa siku nne wa nchi tano za Afrika. Mkutano huo, uliandaliwa na Rais Jamal Abdul Nasser wa Misri. Katika ziara hiyo Mwalimu Nyerere na Mheshimiwa Abeid Karume walitunukiwa uraia wa jiji la Alexandria. Baadhi ya viongozi mashuhuri walotembelea Zanzibar wakati wa uhai wa Abeid Amani Karume ni pamoja na Waziri Mkuu wa Hungary, Bwana Gyula Ka'llai, Makamo wa Rais wa Zambia Reuben Kamanga na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Korea Bwana Kang Ryang. Wengine ni Rais Jamal Abdel Nasser wa Misri, Rais Modibo Keite wa Mali , Rais Makarios wa Cyprus na Rais Tito wa Yugoslavia.

Wengine ni Rais wa Hungary Bwana Pal Losonczi, Waziri Mkuu wa Guyana Bwana Burham na Waziri Mkuu wa Swaziland, Prince Makhosini Dlamini.

Mheshimiwa Abeid Amani Karume, kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar, na mmoja wa waasisi wa Chama cha Afro-Shirazi na Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania aliuwawa akiwa na umri wa miaka 67. Mauwaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Aprili,1972 saa 12.05 za jioni katika jengo la Makao Makuu ya ASP Kisiwandui.

Mara tu baada ya mauaji hayo hali ya hatari ilitangazwa na msako mkali wa wahalifu ulianza nchi nzima. Watuhumiwa kadhaa wakiwemo raia na maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama walitiwa mbaroni, ambapo mtuhumiwa mkuu akiwa ni Abdulrahman Muhammed Babu aliyekamatwa huko Dar es Salaam.

Maziko ya Sheikh Abeid Amani Karume yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kutoka nchi mbalimbali duniani. Wengi wa wageni hao walianza kumiminika Zanzibar kuanzia saa tatu za asubuhi na kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu katika jumba la serikali Forodhani. Baada ya kutolewa heshima za mwisho,jeneza lilitolewa nje na kikosi cha wanajeshi ili kusaliwa katika uwanja wa Ikulu.

Baada ya marehemu kusaliwa hapo Ikulu, jeneza lilichukuliwa hadi Makao Makuu ya ASP Kisiwandui, kupitia barabara ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Makumbusho, Mkunazini na kupindisha kuelekea barabara ya Michenzani hadi Makao Makuu ya Afro-Shirazi.

Hitma ya Abeid Karume ilisomwa katika ukumbi wa klabu ya wananchi tarehe 29 Julai, 1972 wakati wa jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kadhaa. Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970.

Baadhi ya taasisi ambazo zimepewa jina la Karume ni Chuo cha Ufundi cha Mbweni Zanzibar, Kiwanja cha Ndege cha Chake Chake Pemba, Viwanja vya mpira vya Musoma na Dar es Salaam na Kituo cha Televisheni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970. Jumba hilo la kwanza liligharimu jumla ya Shilingi milioni 4,752,000/-. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikusudia kujenga fleti 7000 katika mji wa Zanzibar na kutoa nafasi za makazi kwa wananchi 30 Elfu.

Tuesday, April 4, 2017

Suluhisho la kukojoa kitandani

Kukojoa kitandani ni tatizo la kawaida miongoni mwa watoto wadogo wakati mwingine wapo hata watu wazima wanaokabiliwa na tatizo hili.

Ni kitendo cha kutokujitakia cha kutoa mkojo ukiwa usingizini kitandani. Ingawa ni jambo linalohuzunisha sana hata hivyo ni jambo la kawaida kwa watoto wadogo mpaka miaka 6.

Watoto huwa hawafanyi kitendo hiki kwa kujipendea au sababu ni wavivu, hapana, ni matatizo yaliyopo kwenye kibofu cha mkojo ikiwemo:

Kuwa na kibofu kidogo cha mkojoKuchelewa kukua au kukomaa kwa kibofu cha mkojoUzalishwaji uliozidi wa mkojo,U.T.I ( yutiai)Mfadhaiko (stress)Kufunga choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu kwa kipindi kirefuUsawa usiosawa wa homoni.

Watoto kwa kawaida hupata usingizi mzito sana kila siku sababu ya michezo yao ya kutwa nzima na hivyo ubongo wao haupati ishara za kutosha za kibofu cha mkojo kujaa. Pia katika baadhi ya watoto tatizo la kukojoa kitandani huweza kuwa ni jambo la kurithi toka kwa wazazi wao.

Kadri mtoto anavyokuwa mkubwa ndivyo na tatizo la kukojoa kitandani linavyopungua. Wakati mwingine hili linaweza kuendelea hata ukubwani na hivyo kuwa shida kwa mtoto mwenyewe, wazazi wake na jamii inayomzunguka kwa ujumla.

Unaweza kumsaidia mwanao aache kukojoa kitandani kwa kutumia baadhi ya dawa hizi asili 8 hapa chini, chagua inayopatikana kirahisi mahali ulipo na uitumie, hata hivyo dawa namba 1 ni mhimu itumike sambamba na nyingine moja au mbili kwa matokeo mazuri zaidi.

Dawa za asili 8 zinazotibu tatizo la kukojoa kitandani

1. Maji ya Kunywa
Ikiwa mtoto au hata mtu mzima mwenye tatizo hili atakunywa maji kabla ya kwenda kulala (ndiyo namaanisha kabla ya kwenda kulala usidhani nimekosea) basi hataweza kukojoa kitandani tena akiwa usingizini.

Kile unatakiwa kufanya ni kunywa maji mengi zaidi kila siku kutwa nzima kidogo kidogo.

Kukojoa kitandani hutokea wakati kibofu cha mkojo kinazalisha hydrogen na nitrogen kwa pamoja na kuunda amonia. Amonia ni sumu katika mwili wa binadamu. Wakati ubongo unapopata ujumbe kutoka kwenye kibofu cha mkojo, ubongo humfanya mtoto aote kwamba yupo chooni na hatimaye hukojoa akiwa usingizini.

Huku yupo usingizi bado ataona wazi yupo chooni sababu ya hiyo ammonia.
Kwahiyo sababu ya mtu kukojoa kitandani ni matokeo ya kuundwa kwa amonia kwenye kibofu cha mkojo na amonia hii inaondolewa kirahisi mwilini kwa kunywa maji mengi kila siku.

Watu wengi hawanywi maji ya kutosha kila siku, wengi kama siyo wote wanasubiri KIU ndipo wanywe maji jambo ambalo ni kosa. Kiu ni ISHARA ya mwili iliyoCHELEWA ya kuhitaji maji.

2. Mdalasini
Mdalasini ni dawa rahisi zaidi kwa mtoto anayekojoa kitandani. Inaaminika kwamba kiungo hiki huufanya mwili kuwa wa moto moto.

Chukua mdalasini ya unga kama kijiko kidogo kimoja hivi cha chai changanya na asali kijiko kidogo tena na upake kwenye kipande cha mkate na umpe mtoto ale kila siku wakati wa chai ya asubuhi

3. ZabibuBata (Indian Gooseberry)
ZabibuBata ambazo pia hujulikana kama amla ni dawa nyingine ya kihindi nzuri kwa ajili ya tatizo hili la kukojoa kitandani.

Chukua zabibubata 2 kisha ondoa ganda lake la nje na uziponde kidogo, halafu changanya pamoja na kijiko kidogo cha chai cha asali na kiasi kidogo cha binzari ya unga. Mpe mtoto kijiko kidogo cha chai cha mchanganyiko huu kila siku asubuhi mpaka atakapopona.

4. Masaji
Masaji pia inatibu tatizo la kukojoa kitandani na kwa matokeo mazuri zaidi tumia mafuta ya zeituni (olive oil).

Yapashe moto kidogo mafuta ya zeituni ili yawe ya uvuguvugu kwa mbali na upake ya kutosha sehemu ya chini ya tumbo la mtoto na ufanye masaji eneo hilo polepole kwa dakika kadhaa.

Fanya zoezi hili kila siku mpaka umeridhika na mtokeo yake.

5. Jozi (Walnuts) na ZabibuKavu (Raisins)
Jozi na Zabibu kavu vinaweza pia kutumika kupunguza tatizo la kukojoa kitandani. Watoto wengi watafurahia pia kutumia kwani hivi ni vitu vya asusa (snack).

Mpe mtoto jozi 2 na zabibu kavu 5 kabla ya kwenda kulala kila siku kwa wiki kadhaa mpaka umeanza kuona mabadiliko.

6. Asali mbichi
Dawa nyingine maarufu kutibu tatizo la kukojoa kitandani ni asali mbichi. Watoto wengi wanapenda radha tamu ya asali na hivyo ni rahisi kutumika kwao kama dawa.

Mpe mtoto kijiko kidogo kimoja cha chai cha asali mbichi kila anapoenda kulala kila siku mpaka atakapopona. Unaweza pia kuchanganya na maziwa fresh wakati wa chai ya asubuhi.

7. Siki ya tufaa (Apple Cider Vinegar)
Siki ya tufaa husaidia kuweka sawa usawa wa asidi na alkaline mwilini (body’s Ph) na hivyo kupunguza asidi iliyozidi katika mwili kitu ambacho kinaweza kuwa ni moja ya sababu za tatizo la kukojoa kitandani.

Siki ya tufaa pia husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini pia hutibu tatizo la kufunga choo vitu vingine ambavyo husababisha tatizo la kukojoa kitandani.

Mimina vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya kunywa na umpe mtoto anywe kutwa mara 1 kila siku, unaweza pia kuongeza asali kidogo ndani yake kupata radha. Vizuri akinywa wakati wakula chakula cha mchana au cha jioni.

8. Mbegu za Mharadali (Mustard Seeds)
Dawa nyingine nzuri kwa tatizo la kukojoa kitandani ni mbegu za mharadali. Ni dawa nzuri pia kwa wale wenye tatizo la U.T.I (yutiai).

Weka nusu kijiko kidogo cha chai cha mbegu za mharadali au unga wa mbegu hizi ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha maziwa fresh asubuhi na umpe mtoto anywe kinywaji hiki lisaa limoja kabla ya kwenda kulala kila siku mpaka amepona.

Mambo ya mhimu kuzingatia ili ufanikiwe na dawa hizi:
• Wasiwasi na mfadhaiko (stress) huweza kuongeza ukubwa wa tatizo. Hivyo badala ya kumkalipia au kumdhalilisha kila siku mtoto muonyeshe upendo na uwe tayari kumsaidia polepole mpaka anapona tofauti na hapo tegemea tatizo kutokuisha kwa haraka.

• Mhimize mtoto kwenda kukojoa kabla ya kwenda kulala kila siku

• Hakikisha kuna taa au mwanga wa kutosha njia ya kuelekea chooni, wakati mwingine mtoto akiona giza anaogopa kwenda chooni hasa kama choo kipo mbali na anapolala hasa kwenye nyumba zetu hizi za uswahilini.

• Mpe zawadi yoyote ndogo kila siku anapofanikiwa kuamka salama bila kukojoa kitandani, hii itamuongezea nguvu na moyo zaidi wa kujidhibiti zaidi na tatizo lake.

• Dhibiti matumizi ya juisi hasa juisi zenye sukari nyingi na za dukani nyakati za jioni.

• Epuka vinywaji vyenye kaffeina kama vile chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi, malta, energy drinks zote na vingine vyote vyenye kaffeina ikiwemo chokoleti

• Tibu tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

• Tumia karatasi linalozuia maji kupenya kwenye godoro moja kwa moja ili
kupunguza harufu mbaya chumbani na usumbufu usio wa lazima.

• Weka alamu muda ule unaona mara nyingi mtoto ndiyo hujikojolea, weka saa yenye kengele (alarm) muda huo ili aweze kushtuka kabla na aende chooni.

Tatizo la kukojoa kitandani si tatizo linaloweza kutibika kwa haraka haraka ndani ya siku 2 au 3. Kuwa mvumilivu na mpole, walau jaribu tiba kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na usikate tama haraka.  

Saturday, April 1, 2017

Muendelezo wa njia za kuondoa sumu mwilin


9. Pata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni  pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.

Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo kama kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.  Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!

10. Epuka mazingira hatarishi kwa sumu

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

11. Tumia mtindi

Moja ya njia nyingine ya kuondoa sumu na takataka nyingine ni kutumia vyakula vyenye bakteria wazuri (probiotics). Mtindi ndicho chakula pekee kinajulikana kuwa na bakteria hawa wazuri kwa ajili ya tumbo lako. Pata mtindi kikombe kimoja kila siku na utabaki na mwili msafi muda wote.

Tumia mtindi wa nyumbani ndiyo mzuri zaidi ingawa hata wa dukani nakuruhusu utumie hasa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake (flavors and additives).

12. Epuka vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.

13. Ondoa mfadhaiko (stress)

Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress. Kama utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua. Vitu viwili vinaondoa stress bila kulazimika kutumia njia mbaya kwa afya yako ni mazoezi ya viungo na tendo la ndoa. Siku nyingine ukijiona umefadhaishwa sana nenda kafanye mazoezi ya kufa mtu ikiwezekana baadaye tafuta mtu shiriki tendo la ndoa.

14. Tumia dawa za asili badala ya zile za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya. Kama unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

15. Acha vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi kama pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.

Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha. Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha kama tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

16. Tumia vifuatavyo kuondoa sumu zaidi

Vifuatavyo vinaondoa sumu kirahisi zaidi mwilini; kitunguu swaumu, unga wa majani ya mlonge na mbegu zake na mbegu za maboga au unga wake.
Kitunguu swaumu
Mlonge
Mbegu za maboga

Thursday, March 30, 2017

ONDOA SUMU MWILINI KWA NJIA zifuatazo

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng'enyo wa chakula mwilini mwako.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

-Uchovu sugu
-Maumivu ya maungio
-Msongamano puani
-Kuumwa kichwa kila mara
-Tumbo kujaa gesi
-Kufunga choo au kupata choo kigumu
-Kukosa utulivu
-Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
-Pumzi mbaya
-Mzunguko wa hedhi usio sawa
-Kuishiwa nguvu
-Kushindwa kupungua uzito
-Kupenda kula kula kila mara

Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini

1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee

Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi. Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee.

2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani

Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani  au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Fanya masaji

Kwa bahati mbaya waTanzania wengi hawajuwi kuwa masaji ni sehemu ya tiba au ni dawa pia kwa magonjwa mengine mengi mwilini. Wengi tunaichukulia masaji kama kitu cha starehe tu (relaxation) lakini unaweza kutumia masaji kama njia mojawapo ya kuondoa sumu mwilini na utafanikiwa kwa muda mfupi sana.

4. Kunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni. Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo. Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo ili kusafisha damu na mwili kwa ujumla ni lazima unywe maji ya kutosha kila siku.

5. Acha chai ya rangi na Kahawa

Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa. Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai. Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake. Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

6. Fanya mazoezi ya viungo

Inashangaza sana kuona waTanzania wengi hawaoni umhimu wa kufanya mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo ni jambo la lazima kama ilivyo chakula. Iwe unaumwa au huumwi, iwe una uzito kuzidi au una uzito wa kawaida hakikisha unapata muda wa kufanya mazoezi.

Mazoezi yanakusaidia kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kukuondolea mfadhaiko au stress kirahisi zaidi, sambamba na hilo mazoezi ni dawa tosha na nzuri ya kuondoa sumu mwilini haraka zaidi. Hakikisha jasho linakutoka la kutosha na iwe ni jambo la kila mara na siyo unaenda jumamosi na jumapili (weekend) tu, hiyo haitoshi, fanya mazoezi mara 4 mpaka mara 5 kwa wiki.

7. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (faiba)

Umesikia mara nyingi kwamba unahitaji kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa ajili ya kuwa na afya bora, mmeng’enyo wa chakula wenye afya na hata kukusaidia kupunguza uzito. Kile ulikuwa hujuwi pengine mpaka sasa ni kuwa vyakula hivi vyenye nyuzinyuzi ni vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu au takataka mbalimbali.

Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho, mchele wa brown (ule wanashauriwa watu wa kisukari wautumie), maharage meusi, njegele, tende, viazi vitamu, tufaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano ambao haujakobolewa.

8. Funga kula

Ndiyo, kama ulikuwa hujuwi namna nyingine rahisi ya kuondoa au kupunguza sumu mwilini ni kufunga kula kabisa kutwa nzima. Ukifunga kula mwili unalazimika kuvitumia vile vilivyomo ndani yake bila kushughulika kuvisaga vingine vipya unavyokula. Kunapokuwa hakuna shughuli ya kuvisaga na kumeng'enya chakula kipya mwilini ndipo mwili unaweza kuondoa sumu na taka nyingine kirahisi zaidi.

Amua kufunga kula kabisa kwa wiki mara 2 hata 3 ili kuondoa au kupunguza sumu, hii inaweza kuwa pia ni njia mojawapo ya kufanya maombi na kujiweka karibu na muumba wako.

TABIA ZA BLOOD GROUP B

Muendelezo.....wa blood group kama ifuatavyo...

Blood group"undefined"

Nb:...Hawa watu huwa Tabia zao hazielewek wanatabia yakubadilika badilika kama kinyonga na ngumu sana kuish na MTU.

Blood group B..."balanced ".
1=ma MC wengi wapo group B.

2= Wasanii/waimba.

3=Waongeaj sana.

Nb:...hawa watu Mara nying huwa wanaweza kuish na MTU yeyote kutokokana aina ya blood Group.

Wednesday, March 29, 2017

TAMBUA TABIA ZA BLOOD GROUP A

Habar ya mda huu,

Leo tujifunze kuhusu Tabia na aina ya Damu group A.

1=Tabia ya watu wenye group A huwa ni wabinafs sana,Anaweza akawa anafaham kitu lakin kakaa nacho tuu na asimshirikishe MTU yaan ni wabinafs sana.

2=Wapole,Na kutokana na hii hali au aina ya group LA dam huwapelekea kuwa na hasira sana na hasira zao huwa haziish yaan ( kinyongo).mnaweza kugombana Leo ukamuomba msamaha baada ya mwaka moja akaja kukukumbusha kuwa kuna siku ulimfanyia kitu fulan,huwa hawasahau.

3=Wanafata sana sheria.

4=wanapenda sana details,kwa mfano watu wenye group A unaweza kumtuma Dukan ukamwandikia kwenye karatas anunue hiki na hiki lakin akifika Dukan anaweza tena kukupigia hivi ulisemaje ni nunue ni Na nin.

5=Hawapend shida.

Sasa changamoto inakuja huyu MTU mwenye group A anapokutana na MTU Wa group 0 huwa shida sana,kwasababu group A ni Wapole wanapenda kuelekezwa kimoja kimoja wakati group 0 huwa ni wababe sana na huwa hawapend kurudia rudia vitu,akishasema amesema.

Kwa hiyo ukiangalia hata kwenye mahusiano MTU Wa Group A ni ngumu sana kuish na group 0.MTU mwenye group O hakawii kukwambia usinisumbue,acha yaan huwa hawapend usumbufu usumbufu hasa wanapokutana na group A.

Monday, March 27, 2017

MADHARA YA POMBE KIAFYA

Pombe za aina ya kinywaji ambacho kinapendwa sana katika jamii, hata hivyo licha ya kuwepo kwa taarifa ya kwamba pombe huongeza furaha ya moyo,  na kuzuia matatizo yatokanayo na msongo wa mawazo, tafiti mbalimbali zinasema ya kwamba pombe zina aina zote kemikali ambazo baadhi ya hizo kemikali huwa ni katika mwili wa mwanadamu.

Labda kwa dakika chache tuangalie matatizo yatokanayo na utumiaji wa pombe.

1;Vidonda vya tumbo.
2;Kansa ya utumbo.
3;Kusinyaa kwa Ini.
4;Kansa ya Ini.
5;Kansa ya umio(oesophagus)
6;Vindonda kwenye mapafu.
7;Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni
.Matatizo ya ganzi miguuni na mikononi(Peripheral Neuropathy).
8.Kisukari.
9;Figo kushindwa kufanya kazi.(Renal failure)
10;Kansa ya figoKukosa au upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.
(Loss of Libido)
12;Upungufu wa nguvu za kiume.
           Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa kama vile Kifua Kikuu,
   1;Kansa,
    2;KisUkari,
     3;Shinikizo la damu la kupanda.
    3;Kukosa hamu ya kula.
(Anorexia)
4; Kutovyonzwa vyema kwa chakula(Malabosorption)
Ugonjwa wa kongosho.(Pancreatis).
          Kichaa cha pombe(mtu hawezi kufanya kazi bila ya pombe,au anakuwa kama mgonjwa lakini akipewa pombe tu anakuwa mzima)
Jambo la muhimu ni kuhakikisha unaepuka utumiaji wa pombe ila kuepuka matatizo niliyoyatabainisha hapo awali.

HISTORIA YA CHIFU WA WAHEHE MKWAWA 1

Mkwawa alikuwa chifu wa wahehe na kiongozi mkuu wa kabila la wahehe ambaye alizaliwa mwaka 1855 -1898 katika kijiji cha Lungemba mkoani Iringa. 

Baba yake mzazi ni Mzee Munyigumba.Baada ya kuzaliwa Mkwawa alipewa jina la 'Ndasalasa' yaani ikiwa na maana ya kupapasa papasa. Alipoofikisha umri wa miaka 23 ulitokea uvamizi ambapo baba yake mzazi Mzee Munyigumba alivamiwa na Wangoni.

Baada ya kuvamiwa Mzee Munyigumba alikimbilia mlima wa Nyamulenge. Alipokuwa pale mlimani Wangoni walimzingira kila pande hivyo Mzee Munyigumba aliamua kuingia pangoni, baada ya kuingia pangoni Wangoni waliamua kuchoma moto pale pangoni ili basi Mzee Munyigumba afie ndani ya pangoni lakini mpango wao haukutimia kwani Mkwawa aliwahi kumuokoa baba yake. 

Mzee Munyigumba alimsifu sana mtoto wake kwa ushujaa alioufanya wa kumkomboa hivyo alimtunuku jina la kishujaa yaani aliitwa "Mkwava Mkwavinyika".

Mapigano kati Mkwawa akiwa na wafuasi wake wa kabila la Wahehe dhidi ya Wangoni yalipamba moto sehemu ya Makambako ambapo Wangoni walishindwa na kuamua kukimbia.

Licha ya Wahehe kushinda lakini bado waliwasifu Wangoni kwa mapigano waliyoyaonesha wakisema kuwa " Leo tumekutana na Makambako" ikiwa na maana kuwa wamekutana na madume hivyo sehemu hiyo tangu siku hiyo ikawa inaitwa Makambako mpaka leo hii.

Lakini baada ya kumaliza mapigano dhidi ya Wangoni, Mkwawa na kikosi chake walirudi Iringa mjini. Kwa bahati mbaya alisikia taarifa mbaya kwamba baba yake amefariki hivyo ilibidi baba yao mdogo Mzee Mwaije agawanye nchi ambapo upande wa kusini alipewa Mkwawa na upande wa kasikazini alipewa Muhenga. Baada ya kupewa maeneo hayo Shemeji yao Mwambambe mwalinyungu ambaye asili yake ni mtu wa Tabora aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga. 

Mwambambe alifika Iringa wakati akiwa Mdogo sana hivyo baba yake Mkwawa alikuwa akimtumia kwenda kuchukua dawa za kichifu na dawa za kivita wakati wakiwa njiani pale walipotokea maadui Mwambambe alikuwa na nguvu za ajabu alikuwa na uwezo wa kumkamata adui mmoja kila upande na kuwagonisha vichwa mpaka wanafariki hivyo baba yake Mkwawa pamoja na wahehe wote kiujumla walimpenda sana Mwambambe kufuatia sifa hizo Mzee Munyigumba alimpatia binti yake amuoe. Hivyo Mwambambe aliwagombanisha Mkwawa na Muhenga kwa kumwambia Muhenga kwamba amepata eneo dogo kuliko Mkwawa hivyo alimwambia kuwa yeye yupo tayari kumsaidia ili apate eneo kubwa.

Wakaanzisha vita ya kumpiga Mkwawa hivyo Mkwawa alitoroka kuelekea Dodoma, wakati akiwa huko baba yake Mdogo aliyekuwa akiishi huko alimuuliza kuwa nchi kamuachia nani? Ilibidi Mkwawa amueleze kilichotokea na kumalizia kwamba amemuachia Mdogo, hapo ndipo baba yake Mdogo alipomwambia inabidi arudi Iringa kwa ajili ya kupambana kwani yule Mdogo wake pia anaweza kupigwa na Mwambambe akachukua nchi na Mwambambe asili yake ni mtu wa Tabora hivyo nchi itakuwa ya watu wa Tabora.

Basi ilibidi Mkwawa arudi Iringa kupambana na hao ndugu zake. Lakini kwa bahati mbaya hawa ndugu zake walishasababisha mauaji, walishinikiza mpaka mama yake Mkwawa alijiua. Baada ya Mkwawa kukimbilia Dodoma walimkamata mama yake na kumlazimisha awaoneshe dawa ya uchifu ambayo ilikuwa inaitwa "LIHOMEO" baada ya kuwa amelazimishwa sana mama Mkwawa aliamua kuwaambia kuwa dawa hiyo inapatikana sehemu inayoitwa Kikongoma hivyo waliondoka kuelekea huko Kikongoma kuchukua dawa. Walipofika Kikongoma walienda mpaka kwenye daraja la Mungu baada ya kufika hapo mama Mkwawa aliwaambia kuwa "Nimefika sehemu ilipo dawa lakini mashariti yake ni lazima nivue nguo ndipo niweze kuichukua hiyo dawa, sasa nyinyi ni wanangu nitavuaje nguo mbele yenu?" Hivyo wale jamaa ilibidi wawatume wamama wawili waende naye wao wenyewe walibaki nyuma kidogo.

Mama Mkwawa alisogea hadi karibu na daraja la Mungu sehemu ambapo kulikuwa na jiwe kubwa, mama mkwawa alivua nguo zake zote na kuziweka juu ya lile jiwe kisha akaanza kulizinguka lile jiwe Mara kadhaa halafu akajirusha ndani ya maji huku akisema, "Mwambambe ulitaka nikuoneshe dawa ili umuue mwanangu umenikosa". Alizungumza kwa lugha ya kihehe kisha akajirusha ndani ya ule mto.

Sunday, March 26, 2017

CHAKULA MUHIMU KWA MJAMZITO

Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili kwa ujumla.

Na endapo mama mjamzito atakosa mlo bora uliombatana na protini anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri

Hivyo ili kujenga afya ya mama na mtoto imeshauriwa ya kwamba mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ili kuweza kupata afya bora:

1.Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa:
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

Mayai:
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A ambayo itasaidia kuzuia infections.

Vyakula vyenye Protein
Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka, uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.

Mboga za majani.
Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya kutosha).  Mboga hizi zitakupa Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata anemia.

Vyakula vyenye vitamin C.
Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu, machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.

Maji ya kunywa.
Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.

Tumia chumvi kiasi.
Chumvi  kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha miguu kuuma na uchovu.

Kwenye sehemu ya pili tutaongelea virutubisho kadhaa na umuhimu wake kwa mama mjamzito na mtoto. Ila kumbuka utumiaji wa chumvi kwa wingi una madhara kiafya.

Saturday, March 25, 2017

FAIDA Za TUNDA LA STAFELY

1.  Majani yake hutumika kama chai na kutibu kuharisha damu, mafua na husaidia mfumo wa umeng'enyaji  wa chakula.

2.  Mizizi yake huua minyoo kwa aina zake .

3.  Mbegu hutengenezwa dawa ya kula na kufukuza wadudu waharibifu.

4.  Tunda ni chanzo kikuu cha  vitamin C , Iron, Niacin Riboflavin na asilimia 12% ya tunda hili ni sukari salama.

5.  Tunda hili pia ni chakula,unaweza kutengeneza juice tamu kwa familia .

Ushauri 
Mgonjwa wa saratani anapokuwa kwenye Tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana Stafeli ili kumpunguzia makali ya dawa za Saratani pamoja na kupunguza maumivu.
Tukumbuke maumivu ya saratani ni maumivu makali kuliko na wagonjwa wanapewa zile dawa kali sana  za maumivu.
Matumizi ya tunda hili yatampunguzia mgonjwa madhara ya dawa.

Kwanini usilifanye tunda hili kuwa Rafiki kwako na familia yako?
Nashauri kila mmoja wetu apande mti japo mmoja wa tunda hili  nakujipatia faida bila kutumia gharama kubwa ya kununulia, Miili yetu inahitaji tunda hili kwa wingi.

Stafeli majina yake mengine ni  Soursop au Graviola.

FAIDA Za TUNDA LA STAFELY

1.  Majani yake hutumika kama chai na kutibu kuharisha damu, mafua na husaidia mfumo wa umeng'enyaji  wa chakula.

2.  Mizizi yake huua minyoo kwa aina zake .

3.  Mbegu hutengenezwa dawa ya kula na kufukuza wadudu waharibifu.

4.  Tunda ni chanzo kikuu cha  vitamin C , Iron, Niacin Riboflavin na asilimia 12% ya tunda hili ni sukari salama.

5.  Tunda hili pia ni chakula,unaweza kutengeneza juice tamu kwa familia .

Ushauri 
Mgonjwa wa saratani anapokuwa kwenye Tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana Stafeli ili kumpunguzia makali ya dawa za Saratani pamoja na kupunguza maumivu.
Tukumbuke maumivu ya saratani ni maumivu makali kuliko na wagonjwa wanapewa zile dawa kali sana  za maumivu.
Matumizi ya tunda hili yatampunguzia mgonjwa madhara ya dawa.

Kwanini usilifanye tunda hili kuwa Rafiki kwako na familia yako?
Nashauri kila mmoja wetu apande mti japo mmoja wa tunda hili  nakujipatia faida bila kutumia gharama kubwa ya kununulia, Miili yetu inahitaji tunda hili kwa wingi.

Stafeli majina yake mengine ni  Soursop au Graviola.

Friday, March 24, 2017

TIBA TOSHA YA MBEGU ZA MABOGA

Watu wengi hupenda zaidi ya kula boga kuliko mbegu zake. Wengi hufanya hivi kwa sababu huona hazina faida kwa kuwa wanavutiwa na boga zaidi, hii sawa nakusema watu hupenda zaidi mnofu kuliko kula mifupa, lakini ukweli ni kwamba mbegu za maboga ni za muhimu sana kwani zina wingi protini na madini ya kutosha ambayo ni muhimu sana katika miili yetu.

Madini ambayo yanapatikana katika mbegu za maboga kama vile zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10  na magonjwa hayo ni kama:

1.Magonjwa ya moyo.
Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa muhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.

2. Husaidia uzalishaji wa maziwa kwa wingi kwa kina mama wanaonyonyesha.
Hivyo kwa mama anenyonyesha anashauriwa kutumia  mbegu za maboga kwa wingi ili kuzalisha maziwa kwa wingi.

3. Huongeza uwezo wa macho kuuona vizuri.
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.

4.Husaidia kuondokana na matatizo ya unene unaotokana na wingi wa mafuta ( cholestrol) mwilini.

5.huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo

6.Husaidia kurekebisha sukari mwilini na kuwezesha kongosho kufanya kazi yake vizuri.

7. Huondoa sumu mbalimbali mwilini na hasa kwenye figo.

8.Husaidia kuondoa shinikizo la damu.

9. Ni kinga dhidi ya kansa ya kizazi kwa wanaume na wanawake.

10. Huboresha akili na kumbukumbu kwa watoto na watu wazima ( kazi ya zinc na omega 3 Fatty).

Hivyo kila wakati inashauriwa kutafuna mbegu hizi zikiwa mbichi kuliko zikiwa zimechemshwa au kukaangwa,  kwani ukitumia ambazo zimechemshwa au kukaangwa kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza baadhi ya vitamini.

Thursday, March 23, 2017

Fursa zituzungukazo

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na           Makampuni mbalimbali.
5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa       vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa           vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
       ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL,          AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,                 vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

Monday, March 20, 2017

KUWA MAKINI KATIKA KUOSHA NYWELE ZAKO


Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

FAIDA YA TANGAWIZ KIAFYA

Asante kwa kuendelea kutembelea Mbinuzamafanikio.blogspot.com, kwani tunaamini ya kwamba unaimarika sana kifkra kupitia makala hizi. 

ambo la msingi katika makala ambazo unazisoma kupitia ukurasa huu unatakiwa kuchukua hatua, hii itakuwa njia bora zaidi la kuweza kutimiza lile kusudio lako.

Tukiachana na hayo naomba nikukaribishe katika Makala haya, kwani siku ya leo tutazungumzia umuhimu wa tangawizi katika kutibu magonjwa mbalimbali. Kwani naamini kila mmoja wetu anaifahamu vyema tangawizi.

Zifuatazo ndizo faida za tangawizi.

1. Tangawizi hutibu matatizo ya koo pamoja na kukauka kwa sauti.

Unachotakiwa kufanya ni:
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.

2. Tangawizi huzuia kichefuchefu na kutapika.

Unachotakiwa kufanya:
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi.

3.Husaidia kutibu maumivu makali ya tumbo.

Unachotakiwa kufanya ni :
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.

4.Tangawizi husaidia kwa kiwango kikubwa matitizo ya kuuma kwa meno pia husaidia kutibu maumivu ya kichwa.

Unachotakiwa kufanya ni:
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.

6. Hutibu mafua makali na kikohozi, osha na kisha

Unachotakiwa kufanya ni :
Twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.
Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili na mafua yatapona kabisa.

Lakini kabla akaweka nukta matumizi mengine ya  tangawizi ni kurekebisha matumizi ya kina mama katika zile siku ngumu. Mathalani, iwapo tarehe zinabadilika mara kwa mara unaweza kutumia kurekebisha mwenendo wa siku hizo muhimu.

FAIDA YA TANGAWIZ KIAFYA

Asante kwa kuendelea kutembelea Mbinuzamafanikio.blogspot.com, kwani tunaamini ya kwamba unaimarika sana kifkra kupitia makala hizi. 

ambo la msingi katika makala ambazo unazisoma kupitia ukurasa huu unatakiwa kuchukua hatua, hii itakuwa njia bora zaidi la kuweza kutimiza lile kusudio lako.

Tukiachana na hayo naomba nikukaribishe katika Makala haya, kwani siku ya leo tutazungumzia umuhimu wa tangawizi katika kutibu magonjwa mbalimbali. Kwani naamini kila mmoja wetu anaifahamu vyema tangawizi.

Zifuatazo ndizo faida za tangawizi.

1. Tangawizi hutibu matatizo ya koo pamoja na kukauka kwa sauti.

Unachotakiwa kufanya ni:
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.

2. Tangawizi huzuia kichefuchefu na kutapika.

Unachotakiwa kufanya:
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi.

3.Husaidia kutibu maumivu makali ya tumbo.

Unachotakiwa kufanya ni :
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.

4.Tangawizi husaidia kwa kiwango kikubwa matitizo ya kuuma kwa meno pia husaidia kutibu maumivu ya kichwa.

Unachotakiwa kufanya ni:
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.

6. Hutibu mafua makali na kikohozi, osha na kisha

Unachotakiwa kufanya ni :
Twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.
Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili na mafua yatapona kabisa.

Lakini kabla akaweka nukta matumizi mengine ya  tangawizi ni kurekebisha matumizi ya kina mama katika zile siku ngumu. Mathalani, iwapo tarehe zinabadilika mara kwa mara unaweza kutumia kurekebisha mwenendo wa siku hizo muhimu.

Saturday, March 18, 2017

Namna ya kupata wateja

Katika ushindani wa kibiashara uliopo na mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia, kupata wateja kumekuwa kugumu sana. Hivyo ili ufanikiwe kweli katika biashara inabidi sio tuu uwe na bidhaa nzuri lakini pia ujue namna bora ya kutafuta wateja.

Hata kama una duka la nguo tuu dogo au saluni waweza kuwa umeathirika na namna ambavyo ushindani wa biashara ulivyo. Hivyo katika makala hii utajifunza mbinu ya kisasa kabisa ya kupata wateja wa biashara yako.

Kabla ya kujifunza  mbinu ya jinsi ya kupata wateja unahitaji kujua kwanza kwanini ni ngumu kupata wateja.

Hali ngumu ya kiuchumi : Kuna namna mbili ambapo hali ya kiuchumi inaweza athiri kupatikana kwa wateja. Kwanza kuwafanya wasiwe na uwezo wa kulipia bidhaa yako , na pili kuwafanya wajifikirie sana kuhusu kununua bidhaa zako. Katika yote haya hali ngumu ya kiuchumi inajenga ukinzani wa wewe kujenga ushawishi kwa wateja wako kununua bidhaazako.

Mabadiliko ya teknolojia: Teknolojia inafanya watu wengi zaidi waweze kuwafikia wateja wako ambapo hapo kabla haikua rahisi. Enzi hizo ilikua utengeneze vipeperushi au uwe na hela za kutosha kutangaza redio, kwa tv na kwenye mabango. Ila sasa watu kupitia Facebook, WhatsApp, na Instagram wanaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi. Hata yule mtengeneza keki mtaani kwenu nae yupo Instagram akitangaza keki na mikate yake. Bwana Mangi nae yupo kwa Facebook akitafuta wateja wa kibanda chake cha kuuza vocha za simu na MPESA.

Njia ya kisasa ya kisasa ya kuwapata wateja:

Tumefika wakati ambapo wateja wengi wana taarifa nyingi kuhusu wapi na kwa bei gani bidhaa zinapatikana. Hivyo wewe kuwa tuu na bidhaa fulani au kwa bei fulani hakutoshi kuwa njia ya kuwafikia.

Pia kwakua kuna watangazaji wengi wa bidhaa inakupasa wewe kuwa na namna ya kipekee ya kuwafikia wateja wako bila kuwa kero kwa wateja kama walivyo watu wengine wengi ambao ni wazi kabisa kwa “makelele” yao ya matangazo wanaonekana wazi wanachotaka wao ni kuuza tuu hizo bidhaa waishie zao. Ni ukweli wa kitaalamu katika marketing kuwa watu wengi  hawapendi kujisikia kuwa fulani anawauzia bidhaa. Hata hivyo hivyo haimaanishi kuwa watu hawapendi kununua. Watu hupenda kununua ila hawapendi ile hali ya kuwekwa “kati” na mtu anayejaribu kuwauzia kitu.

Ukichanganya na ukweli huo kuwa watu hawapendi kujisikia wakiuziwa bidhaa, halafu hali ngumu ya uchumi na mabadiliko ya teknolojia yanafanya kuwepo na “makelele” ya wafanyabiashara wengi,  basi wewe unahitaji mbinu ya ziada.

Hivyo basi mbinu ya kisasa ninayozungumzia hapa ni kutengeneza ushirika na wateja kama jamii ambayo itakuamini na kukuona una kitu zaidi ya kutaka tuu kuwauzia bidhaa zako. Kwa mbinu hii unajenga uhusiano na kufikia hisia za wateja wako, unatambua matatizo yao , unakua kweli mshirika wao katika yale ambayo unaona wao wanaweza kunufaika kupitia bidhaa zako hapo baadae.

Kwa mfano kama wewe ni muuza nguo, badala ya kila wakati kuwatangazia tuu mzigo mpya ulio nao, tambua kwanini hawa watu wanunue nguo mpya. Zungumza nao kuhusu hayo mambo. Mfano iwe ni swala la kujisitiri, au unadhani wananunua sana kwa ajili ya kujionyesha kuwa wanaenda na wakati na ni watu wa mitindo, basi waonyeshe unalielewa hilo kwa kutumia mitandao ya kijamii ukipost vitu vinavyoendana na hayo mambo ya mitindo na kuenda na wakati.

Jiweke katika nafasi zao, na uwahudumie vema kihisia kwanza , ukishawaonyesha kuwa wewe unaweza na unajua nini wanataka , hapo ni rahisi kuwaambia kuhusu bidhaa zako ambazo zitawafikisha katika malengo hayo wanayodhamiria.

Kwa mbinu hii unaondoa upinzani wa wateja kutaka kukusikiliza , na unafanya rahisi kwa wao kufanya maamuzi ya kununua bidhaa zako kwakua hawaoni kama unawauzia bidhaa, bali wanaona ni muendelezo wa ukaribu wako na utayari wako wa kuwaona wakijisikia vizuri na kufikia malengo yao.

Katika kutengeneza huo ukaribu wako na wao kupitia machapisho, videos, na picha mbalimbali wenyewe wateja wajisikia utayari wa kukutafuta. 

Namna ya kuandaa mpango biashara (B ussiness plan)

Watu wengi kwa karne ya sasa huishi kwa malengo ya kuwa watu fulani au watu wanaomiliki vitu fulani,yote hayo yanaweza kufanikiwa endapo mtu/watu hao wapo tayari kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kutumia viungo na akili zetu ambazo tumepewa bure na Mwenyezi Mungu bila malipo yoyote.

Kutokana na changamoto tofauti tofauti katika soko la ajira ikiwa sambamba na ufinyu wa upatikanaji wa ajira zenyewe lakini pia maslahi duni, manyanyaso na mateso yanayopatikana sehemu sehemu za kazi, watu wengi kwa sasa wanaona ni bora wafikirie kuitwa WAAJIRI  na si WAAJIRIWA tena.

Pamoja na matamanio hayo, watu wengi wamekutana na changamoto kubwa katika kuanzisha au kuendeleza biashara hizo. Naomba nieleweke wazi biashara si lazima kununua na kuuza,yaweza kuwa ya kuzalisha na kuuza pia, hapa nazungumzia kujenga na kupangisha, kulima na kuuza, utoaji wa huduma uliyosomea n.k.

Yote hayo na mengine mengi utafanikiwa endapo tu utakuwa na MPANGO BIASHARA katika aina yoyote ya biashara unayofanya au unayotaka kufanya. Mtandao huu kwa kutambua juhudi kubwa za wasomaji wake kutaka kujikomboa kiuchumi leo tunakuletea jinsi ya kuandaa MPANGO BIASHARA (BUSINESS PLAN) ILI UFANIKIWE. Huu utakuwa ni mfululizo wa makala mbali mbali za UCHUMI NA BIASHARA PAMOJA NA FURSA MBALI MBALI UNAZO WEZA KUZITUMIA HAPO HAPO UNAPOISHI.

UTANGULIZI

Mpango biashara Biashara ni nyaraka muhimu sana kwa biashara yako kwakuwa inakupa picha ya matarajio ya namna biashara itakavyokuwa. Ukifanya mchanganuo huo kwa ufasaha kama inavyoelekezwa utaweza kutambua kama kweli biashara unayotaka kuifanya itakulipa au la. Pia utaweza kutambua matatizo na changamoto kabla haujaanza biashara.

Mpango Biashara kwa kiwango flani unahitaji utafiti ili kuweza kuandika vema mambo yanayoendana na biashara yako. Mfano unahitaji kufanya utafiti wa soko ili kujua kwa biashara yako ni akina nani hasa watakuwa wateja wako, na kwanini watakuja kununua bidhaa kwako. Pia unahitaji kufanya utafiti wa gharama utakazotumia kuendesha biashara. Pia gharama za ununuzi wa samani pale utapoendeshea biashara yako,kama Meza, Kiti n.k

Mpango Biashara unakuhitaji ujue picha kubwa ya mazingira ya biashara yako pindi utakapoianzisha. Mfano masuala ya Kodi, Masuala ya Kisheria kama vile Sheria za Ajira, Vibali, Uendeshaji wa Biashara n.k.

Na mwisho kama unataka kuandika Mpango Biashara ili ukaombe mkopo, basi fikiria kwa umakini namna ambavyo utakuja kuulipa mkopo husika. Umejipangaje katika usimamizi makini wa biashara yako.

Ufuatao ni mtiririko wa mchanganuo wa biashara.

Jalada la nje: Linahusisha jina la biashara, muda wa mpango (mfano. 2016 – 2020), anuani ya biashara, toleo, jina la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha mchanganuo unaelekezwa kwa nani.

Dibaji: Sehemu hii huandikwa muhtasari wa mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo mathalani, aina ya biashara, bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi, mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa mwaka, soko lengwa, mtaji unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza kunufaika iwapo akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.

Maelezo ya biashara: Dira/ndoto, madhumuni, historia fupi ya biashara, bidhaa au huduma inayotolewa kwa mapana, uchanganuzi wa hali ya tasnia kwa sasa na siku zijazo, uchanganuzi wa hali ya biashara kwa kuainisha upungufu na nguvu ndani ya biashara, fursa na vihatarishi katika mazingira yanayoizunguka biashara.

Masoko: inazungumzia hali ya soko katika tasnia ya biashara husika, soko unalopanga kuuzia bidhaa au huduma, unaweza kuchukua nafasi gani katika soko hilo kwa asilimia.

Mbinu unazotumia kufikisha bidhaa au huduma kwenye soko, mpango wa mauzo kwa mwezi, kwa mwaka hadi muda wa mpango uliojiwekea mathalani miaka 3 hadi miaka 5, mpango wa bei, hali ya ushindani, mbinu za kuendana na ushindani katika soko, namna ya kutangaza biashara, na unapaswa kuangalia ni jinsi gani utaweka kipaumbele katika kutangaza bidhaa kama una zaidi ya bidhaa moja.

Menejimenti na Utawala: Mfumo wa biashara kama ni ya mtu mmoja, ubia au kampuni, chora chati ya mtiririko wa madaraka, wasifu wa maofisa wa ngazi za juu mathalani Mkurugenzi Mtendaji na wakurugenzi wengine, idadi ya wafanyakazi kwa sasa, mpango wa ukuaji au kuongezeka kwa wafanyakazi, mfumo wa umiliki kama ni kampuni-weka mchanganuo wa hisa za kila mmliki, kama ni ubia elezea mchango wa kila mmoja na namna ya kugawana maslahi, toa mchanganuo kwa wataalam mbalimbali unaowatumia katika biashara mathalani mshauri wa biashara, mwanasheria, wasafirishaji na wakaguzi.

Masuala ya Fedha: Weka makisio ya mizania, mapato na matumizi na mtiririko wa fedha kwa muda wa mpango tangu sasa.

Maelezo ya dhana ya kifedha iliyotumika kupanga makisio, muundo wa mtaji (ainisha kiasi cha mtaji binafsi, msaada, mikopo, na njia nyinginezo kama zipo).

Mwisho ni mpango wa kupata fedha kama zinatoka kwa wawekezaji au benki- kiasi gani unahitaji kwa muda gani na namna gani utalipa kwa faida gani.

Mchanganuo wa vihatarishi vya biashara: Ainisha vihatarishi vya biashara yako, fursa za kibiashara zinazoendena na vihatarishi hivyo, mchanganuo wa itakuwaje endapo mipango uliyojiwekea haitatekelezeka, mchanganuo vihisishi, kwa mfano namna gani bei ikipanda au kushuka inaweza kubadilisha mwelekeo wa biashara yako.

Ratiba ya uzalishaji bidhaa au utoaji huduma:  Mara nyingi  ratiba ya uzalishaji inafanywa kwa programu za kinakilishi.

Viambatanisho: Viambatanisho mbalimbali huwekwa kulingana na mtumiaji wa mchangunuo huo mathalani wasifu binafsi wa maofisa wa ngazi za juu, nakala ya vyeti vya usajili, TIN, leseni na vibali vya biashara.

KWA UFUPI VITU  VYA KUZINGATIA KATIKA KUANDAA MPANGO BIASHARA

Muhtasari wa biashara yakoHistoria na maelezo ya biashara yakoMaelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yakoMchanganuo wa masokoUkubwa wa sokoMgawanyo wa sokoAina ya soko/masokoMchanganuo wa ushindaniWatoa huduma au wauza bidhaa kama yakoUdhaifu waoUwezo waoMkakati wa utekelezajiUongozi na usimamizi wa kaziUchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yakoMkakati wa UzalishajiMkakati wa kuuzaMpango wa fedhaUchambuzi wa mahitaji ya mtajiWapi utatoa mtajiMatumizi ya mtajiMakisio ya MauzoUchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)Makisio ya faida au hasaraMakisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)LeseniCheti cha ulipaji kodiCheti cha usajiliTaarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu.