Saturday, March 18, 2017

Namna ya kuandaa mpango biashara (B ussiness plan)

Watu wengi kwa karne ya sasa huishi kwa malengo ya kuwa watu fulani au watu wanaomiliki vitu fulani,yote hayo yanaweza kufanikiwa endapo mtu/watu hao wapo tayari kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kutumia viungo na akili zetu ambazo tumepewa bure na Mwenyezi Mungu bila malipo yoyote.

Kutokana na changamoto tofauti tofauti katika soko la ajira ikiwa sambamba na ufinyu wa upatikanaji wa ajira zenyewe lakini pia maslahi duni, manyanyaso na mateso yanayopatikana sehemu sehemu za kazi, watu wengi kwa sasa wanaona ni bora wafikirie kuitwa WAAJIRI  na si WAAJIRIWA tena.

Pamoja na matamanio hayo, watu wengi wamekutana na changamoto kubwa katika kuanzisha au kuendeleza biashara hizo. Naomba nieleweke wazi biashara si lazima kununua na kuuza,yaweza kuwa ya kuzalisha na kuuza pia, hapa nazungumzia kujenga na kupangisha, kulima na kuuza, utoaji wa huduma uliyosomea n.k.

Yote hayo na mengine mengi utafanikiwa endapo tu utakuwa na MPANGO BIASHARA katika aina yoyote ya biashara unayofanya au unayotaka kufanya. Mtandao huu kwa kutambua juhudi kubwa za wasomaji wake kutaka kujikomboa kiuchumi leo tunakuletea jinsi ya kuandaa MPANGO BIASHARA (BUSINESS PLAN) ILI UFANIKIWE. Huu utakuwa ni mfululizo wa makala mbali mbali za UCHUMI NA BIASHARA PAMOJA NA FURSA MBALI MBALI UNAZO WEZA KUZITUMIA HAPO HAPO UNAPOISHI.

UTANGULIZI

Mpango biashara Biashara ni nyaraka muhimu sana kwa biashara yako kwakuwa inakupa picha ya matarajio ya namna biashara itakavyokuwa. Ukifanya mchanganuo huo kwa ufasaha kama inavyoelekezwa utaweza kutambua kama kweli biashara unayotaka kuifanya itakulipa au la. Pia utaweza kutambua matatizo na changamoto kabla haujaanza biashara.

Mpango Biashara kwa kiwango flani unahitaji utafiti ili kuweza kuandika vema mambo yanayoendana na biashara yako. Mfano unahitaji kufanya utafiti wa soko ili kujua kwa biashara yako ni akina nani hasa watakuwa wateja wako, na kwanini watakuja kununua bidhaa kwako. Pia unahitaji kufanya utafiti wa gharama utakazotumia kuendesha biashara. Pia gharama za ununuzi wa samani pale utapoendeshea biashara yako,kama Meza, Kiti n.k

Mpango Biashara unakuhitaji ujue picha kubwa ya mazingira ya biashara yako pindi utakapoianzisha. Mfano masuala ya Kodi, Masuala ya Kisheria kama vile Sheria za Ajira, Vibali, Uendeshaji wa Biashara n.k.

Na mwisho kama unataka kuandika Mpango Biashara ili ukaombe mkopo, basi fikiria kwa umakini namna ambavyo utakuja kuulipa mkopo husika. Umejipangaje katika usimamizi makini wa biashara yako.

Ufuatao ni mtiririko wa mchanganuo wa biashara.

Jalada la nje: Linahusisha jina la biashara, muda wa mpango (mfano. 2016 – 2020), anuani ya biashara, toleo, jina la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha mchanganuo unaelekezwa kwa nani.

Dibaji: Sehemu hii huandikwa muhtasari wa mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo mathalani, aina ya biashara, bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi, mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa mwaka, soko lengwa, mtaji unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza kunufaika iwapo akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.

Maelezo ya biashara: Dira/ndoto, madhumuni, historia fupi ya biashara, bidhaa au huduma inayotolewa kwa mapana, uchanganuzi wa hali ya tasnia kwa sasa na siku zijazo, uchanganuzi wa hali ya biashara kwa kuainisha upungufu na nguvu ndani ya biashara, fursa na vihatarishi katika mazingira yanayoizunguka biashara.

Masoko: inazungumzia hali ya soko katika tasnia ya biashara husika, soko unalopanga kuuzia bidhaa au huduma, unaweza kuchukua nafasi gani katika soko hilo kwa asilimia.

Mbinu unazotumia kufikisha bidhaa au huduma kwenye soko, mpango wa mauzo kwa mwezi, kwa mwaka hadi muda wa mpango uliojiwekea mathalani miaka 3 hadi miaka 5, mpango wa bei, hali ya ushindani, mbinu za kuendana na ushindani katika soko, namna ya kutangaza biashara, na unapaswa kuangalia ni jinsi gani utaweka kipaumbele katika kutangaza bidhaa kama una zaidi ya bidhaa moja.

Menejimenti na Utawala: Mfumo wa biashara kama ni ya mtu mmoja, ubia au kampuni, chora chati ya mtiririko wa madaraka, wasifu wa maofisa wa ngazi za juu mathalani Mkurugenzi Mtendaji na wakurugenzi wengine, idadi ya wafanyakazi kwa sasa, mpango wa ukuaji au kuongezeka kwa wafanyakazi, mfumo wa umiliki kama ni kampuni-weka mchanganuo wa hisa za kila mmliki, kama ni ubia elezea mchango wa kila mmoja na namna ya kugawana maslahi, toa mchanganuo kwa wataalam mbalimbali unaowatumia katika biashara mathalani mshauri wa biashara, mwanasheria, wasafirishaji na wakaguzi.

Masuala ya Fedha: Weka makisio ya mizania, mapato na matumizi na mtiririko wa fedha kwa muda wa mpango tangu sasa.

Maelezo ya dhana ya kifedha iliyotumika kupanga makisio, muundo wa mtaji (ainisha kiasi cha mtaji binafsi, msaada, mikopo, na njia nyinginezo kama zipo).

Mwisho ni mpango wa kupata fedha kama zinatoka kwa wawekezaji au benki- kiasi gani unahitaji kwa muda gani na namna gani utalipa kwa faida gani.

Mchanganuo wa vihatarishi vya biashara: Ainisha vihatarishi vya biashara yako, fursa za kibiashara zinazoendena na vihatarishi hivyo, mchanganuo wa itakuwaje endapo mipango uliyojiwekea haitatekelezeka, mchanganuo vihisishi, kwa mfano namna gani bei ikipanda au kushuka inaweza kubadilisha mwelekeo wa biashara yako.

Ratiba ya uzalishaji bidhaa au utoaji huduma:  Mara nyingi  ratiba ya uzalishaji inafanywa kwa programu za kinakilishi.

Viambatanisho: Viambatanisho mbalimbali huwekwa kulingana na mtumiaji wa mchangunuo huo mathalani wasifu binafsi wa maofisa wa ngazi za juu, nakala ya vyeti vya usajili, TIN, leseni na vibali vya biashara.

KWA UFUPI VITU  VYA KUZINGATIA KATIKA KUANDAA MPANGO BIASHARA

Muhtasari wa biashara yakoHistoria na maelezo ya biashara yakoMaelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yakoMchanganuo wa masokoUkubwa wa sokoMgawanyo wa sokoAina ya soko/masokoMchanganuo wa ushindaniWatoa huduma au wauza bidhaa kama yakoUdhaifu waoUwezo waoMkakati wa utekelezajiUongozi na usimamizi wa kaziUchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yakoMkakati wa UzalishajiMkakati wa kuuzaMpango wa fedhaUchambuzi wa mahitaji ya mtajiWapi utatoa mtajiMatumizi ya mtajiMakisio ya MauzoUchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)Makisio ya faida au hasaraMakisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)LeseniCheti cha ulipaji kodiCheti cha usajiliTaarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu.

 

No comments:

Post a Comment