Habari za Leo ndg jamaa na rafiki
yangu natumai wote tu wazma.
Karibu tena kwa wakati mwingne katika kuweza kujifunza na kuangalia baadhi ya mambo ambayo yatatuhamasisha kufanya maamuz na kupata mafanikio kila siku.
Ndg yangu Leo napenda kuongelea kuhusiana na NAMNA YA KUANZA SIKU YAKO UKIWA UMEHAMASIKA.
Nikiwa na maana ya kwamba kuanza siku vizuri ambapo ukiwa unaendelea na shughuli zako uweze kulifikisha lengo lako kwa kiasi fulani kwa kila siku.
Je? Ndugu yangu kila uamkapo huwa unapenda kufanya kitu gan ambacho huwa chakuhamasisha kufikia lengo lako?
Natambua ya kwamba kila mmoja kuna staili yake ambayo huwa anaipendelea kuanza nayo siku .
Naomba nikuambie kitu kimoja ambacho ni cha muhimu sana UNATAKIWA KILA UANZAPO SIKU ANZA KWA KUSOMA AU KUANDIKA LENGO LAKO UNALOHITAJI KULIFANIKISHA KWA SIKU HIYO.
Ukifanya hivyo daima utazd kuwa ni mtu mwenye maendeleo na mwenye mafanikio kila siku.
Pia kama ww nisomaji wa magazeti nakuomba usipende kuanza siku kwa gazeti za udaku .kwa maana ukianza na udaku akili yako itakuwa imeanza vibaya kwa maana haujaupa chakula chake kilicho kizuri .lakn ukianza na gazeti ambazo huwa zinakuhamasisha kufanya jambo la mafanikio .
Daima utakuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa sana.
Asante sana napenda niishie hapo na pia naomba uendelee kupitia Mara kwa Mara ili tuweze kujifunza na kuelimishana katika vitu ambavyo vitatuhamasisha kutupa mafanikio.
Nawatakia siku njema
NAPENDA KUKUONA UKIFANIKIWA
BY MR B MWAMPULULE
No comments:
Post a Comment