Wednesday, November 2, 2016

SABABU INAYOKUKWAMISHA MAFANIKIO.

Habari za asubuhi ndg jamaa na rafiki yangu .Natumai wote tu wazma kwa Mara nyingne tumeiona siku ya Leo kwa rehema na neema za MUNGU.

    Ndg yangu siku ya Leo napenda tujifunze na tukifanyie kazi kitu kimoja   ambacho kinaitwa MAAMUZI.
    natambua ya kwamba hili neno tumelisikia sana na kila siku huwa tunalitumia katika maisha yetu ya kila siku.
  Lakn hili neno lina maana nying japo sisi twazitambua chache.
MAAMUZI   ni jambo ambalo ni muhimu sana kwetu sisi binadamu katika kuangalia kutazama na  kutafakari ni jambo gani tufanye hv au tufanye vile kwa maana usipoamua kulifanya huwezi kulifanya.
Mfano fikiria ww ni mzazi ambaye una familia na mke au mume na watoto wawili  ambapo hapo watoto wako wamefikia miaka ya kwenda shule.
   Sasa je ukiamua kuwapeleka shule wanao ili wakapate elimu kujifunza vilivyo ving .utakuwa umesaidia kuondokana na ujinga kwa watoto.
  Lakn je?  Usipoamua kuwapeleka shule watoto wako watakuwa na uelewa wa kiasi gan?
   Kwa hiyo maamuz ya kutaka kufanikiwa yako mikononi mwako na akilini mwako kwa kuweza kuamua ya kuwa sasa mm NATHUBUTU kuanza kufanya jambo fulani na kwa muda fulani .hapo utaweza kufanikiwa kwa maana umeamua kufanya kile UKIPENDACHO NA KUKIONA NDIO NJIA YA KUTOKEA  NA KUKUPATIA MAFANIKIO. 

EWE NDUGU YANGU  NA UFANYE MAAMUZ YALIYO SAHIHI AMBAYO YATAKUPATIA MAFANIKIO KWA NJIA ILIYO HALALI.
  NAPENDA KUONA TUKIFANIKIWA
   NAKUTAKIA SIKU NJEMA
BY MR B .MWAMPULULE

No comments:

Post a Comment