Ugonjwa wa vidonda vya tumbo umekuwa kikwazo kikubwa katika afya za wengi, hii ni kutokana watu wengi wamekuwa wakiumwa ugonjwa huo. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu, au kuna mtu unamfahamu anasumbuliwa na ugonjwa huu nakuhusihi tufuatane pamoja, kwani makala ya leo ni tiba tosha kwa ajili ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
1. Tumia asali mbichi.
Asali mbichi ni miongoni mwa vimininika ambavyo vinatajwa kutibu magonjwa mengi sana ikiwemo vidonda vya tumbo. Asali mbichi nzuri ni ile ambayo haijachakachuliwa kabisa kwani ina uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwani katika asali mbichi ku na kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.
Unachotakiwa kufanya katika matumizi ya asali mbichi ili kutibu vidonda vya tumbo ni:
Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4 mfululizo.
2. Tumia juisi ya kabeji.
Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.
Ambapo inaelezwa ya kwamba licha ya watu kuitumia kabeji kama mboga lakini pia kabeji ni dawa. Kwani Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori.
Unachotakiwa kufanya ni
Chukua kabeji ambayo umekwisha iandaa kisha kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, kisha chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
Baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya kifungua kinywa mida ya asubuhi, pia fanya hivyo kabla ya kula chakula cha mchana, pia fanya hivyo muda wa jioni, lakini usisahau kunywa kikombe kimoja kabla ya kulala.
MUHIMU
Hivyo hakikisha unarudia kuitumia juisi hii freshi na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani kwani juisi nyingi za dukani hazina uasilia, kwani baadhi zimechanganywa na baadhi ya kemikali ambazo zitakuwa ni salama kiafya.
No comments:
Post a Comment