Sunday, March 12, 2017

TIBA YA ALOEVERA

Bila shaka anaufahamu mmea huu, kwani umechukulia umaarufu miaka ya hivi karibuni katika kutibu magonjwa mbalimbali. Japo mmea huu ni miongoni mwa mimea ambayo ni michungu sana hasa ambapo unatumia. Lakini uchungu huo ndio dawa yenyewe.  Lakini wataalamu mbalimbali wanasema ya kwamba ili kuondokana na uchungu huo wanashauri uweze kuchanganya na asali mbichi ambayo hajachakachuliwa.

Ifuatavyo ndiyo kazi ya mmea wa aloe vera katika kutibu magonjwa yafuatayo:

Huondoa sumu mwilini na kufanya utendaji kazi wa mwili urudi katika hali ya kawaida.Haidia kujenga seli mpya baada ya majeraha ya moto, kujikata, michubuko,Aloe beta husaidia kutibu vidonda vya tumbo.Husaidia matatizo ya kutopata haja, pia maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo.Huondoa matatizo ya ngozi kama chunusi (acne) na fangasi.Ni msaada tosha katika umeng’enyaji wa chakula.kuongeza kinga ya mwili dhidi ya mogonjwa mbalimbali.Mmea huu husaidia pia kuondoa maumivu sehemu mbalimbali za mwili, pia husaidia kupunguza uchovu kwa kiwango cha hali ya juu sana.Hutibu matatizo ya kuhara na kutopata haja kubwa kiurahisi.Lakini vilevile aloe vera husaidia wanaume wengi ambao wanaosumbuliwa na matatizo ya kuziba kibofu cha mkojo na pia kinamama wanao sumbuliwa na uambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI).

Namna ya kuandaa mchanganyiko wa aloevera.

katakata vipande vidogovidogo kisha viweke katika maji safi na salama, kisha  subiri mchanganyiko huu kwa muda wa saa moja kisha anza kwa ajili ya matibabu.

Ili kupunguza uchungu, unaweza kutengeneza juisi yake na kuichanganya na asali ya nyuki wadogo.

Matumizi:

Kunywa kila siku kwa muda wa wiki mbili, asubuhi na jioni kabla ya kula chochote. Kwa kutumia kikombe kimoja cha chai. 

No comments:

Post a Comment