Saturday, March 18, 2017

TIBA TOSHA YA KISUKARI KWA KUTUMIA CHAKULA N.A. MAZOEZI

Kwa mgonjwa wa kisukari anashauriwa kuweza kufanya yafuatayo ili kuweza kupunguza kiwango cha sukari katika mwili wake. Kwani inasadikika ya kwamba kwa mgonjwa wa kisukari anatakiwa kuwa na kiwango cha kati cha sukari katika damu, kwani pindi sukari ikipungua sana (Hypoglycemia) au sukari ikizidi (Hyperglycemia) huwa ina athari kubwa kiafya.

Hivyo kwa kuzingatia ushauri mbalimbali wa wataalamu wa afya wanasema ya kwamba, ili kuweza kuweza kufanya kiwango cha sukari kuwa katika hali ya kawaida unashauriwa kufanya yafuatayo:

1. Kula chakula cha wanga kwa wingi.
Mgonjwa wa kisukari hana masharti ya ajabu kuhusu chakula anachotakiwa kula, kimsingi anaweza kula chakula chochote anachopenda. Kuna mambo matatu ambayo yanabidi kuangaliwa katika kuweka kiwango cha sukari cha mgonjwa kwenye kiwango kinachofaa. Mambo hayo ni:

-Ni chakula gani-Chakula hicho kinaliwa kwa kiasi gani-Chakula hicho kinaliwa muda gani

Watalaamu wa afya na mambo ya chakula wanabainisha kwamba chakula kinachotakiwa kuliwa kwa wingi zaidi ni chakula chenye wanga (carbohydrates), kikifuatiwa na mboga na matunda, kisha chakula chenye protini na mwisho ni chakula chenye mafuta (fats).

Tunapozungumzia chakula Chenye Wanga hapa tuna maana chakula ambacho kinapatikana zaidi kati mboga za majani,  nafaka,  matunda pamoja na maziwa ya mgando. Wataalamu wanasisitiza kula chakula hiki cha wanga kwani aina hiyo ya vyakula husaidia katika kuzalisha glucose ambazo husaidia kuweza kujenga nguvu za mwili na kuupa nguvu mwili.

Lakini kama hiyo haitoshi imeshauriwa ya kwamba pindi mtu akila kiasi kile kile cha chakula chenye wanga na muda ule ule kila siku, anakuwa na nafasi kubwa sana ya kudhibiti kiwango chake cha sukari katika mwili wake.

Lakini vilevile tunashauriwa na watalamu wa afya ya kwamba Kuchanganya aina tofauti tofauti za nafaka, matunda na mboga kumeonyesha kusaidia  zinasidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini.

Hivyo ili kuweza kupunguza kiwango cha sukari hakikisha unatumia chakula ambacho nafaka zake ni zile ambazo hazikukobolewa. Na pia matunda hakikisha inayotumia yakiwa na maganda yake. Kwani kwa baadhi ya matunda vitamini yake ipo katika matunda.

Kwa leo naomba tuishie hapo usikose kusoma mwendelezo wa makala haya siku ya kesho, tutazungumzia umuhimu wa mazoezi kwa mgonjwa wa kisukari .

No comments:

Post a Comment